lundi 22 juillet 2013

Kigali: Fuadi & Makenze waweza kujiunga na Kiyovu Sports mwaka huu...

Karim (Kulia) , Fuadi (kushoto).
Wachezaji kutoka Burundi waliotamba miaka ya nyuma kwenye timu ya Vital'o Fc na baadae wakawa wamejiunga na na klabu ya Kiyovu Sports nchini Rwanda,na baada yakuonyesha ujuzi wa hali ya juu wakawa wamesajiliwa na klabu ya Rayon sports walipofanya vyema kwakutwa taji mwaka uliopita kwenye Primus League nchini pale. Duru kutoka Mjini Kigali zinasema kuwa vijana hao wawili wanaweza kujiunga na klabu yao yazamani ya Kiyovu sports ambayo kama mnavyofahamu imeshamsajili Coach mpya Gilbert Kagabo Yaoundé KANYENKORE alie ifunza zaidi ya miaka 20 klabu ya Vital'o kutoka Burundi. Tukimulika zaidi habari hiyo iliondikwa kwenye majarida tofauti nchini Rwanda kama Igihe,inasemekana kuwa vijana hao kwa mdaa huu wapo Mjini Kigali kwa mazungumzo na viongozi wa klabu ya Kiyovu sports waliojiunga nayo mwaka 2009 kabla yakujiunga na Rayon sport. Mwaka 2012, Karim NIZIGIYIMANA alias Makenze ndie alikuwa nahodha (Capitaine) na mwaka 2013 Fuadi Ndayisenga alimrejelea Kanombe aliekuwa anavaa kitamba cha klabu hio. Duru rasmi kutoka Kigali zinasema kuwa klabu ya Kiyovu tayari imewapoteza wachezaji wake nyota wakiwemo Serugaba Eric aliekuwa nahodha,ameamia kwenye klabu ya AS Kigali na Mutarambirwa Djabil naibu wake,ambae yeye amejiunga na klabu ya Police FC. Ifahamike ya kuwa mwaka jana bingwa tetezi wa Primus league ya Rwanda ni Rayon Sport , Burundi zasalia wiki 5 ili bingwa atambulike na hadi mdaa huu ajafahamika kwani timu zinasogeleana sana .

1. Flambeau de l'Est 36 points
2. Atlhetico Olympic 36 points
3. Lydia Ludic Burundi Academie 34 points
4. Vital'o fc 32 points (-1 match)
5. Royal fc 28 points
 Kwa upande wa ligi , wiki hii hapakuwepo mchuano hata umoja, wameichukuwa na fasi kwa kuwapa wachezaji wa timu ya taifa kujinowa vilivyo ili kukabiliana na mahasimu wao wa Mamba za Nil ifikapo Jumaa-pili Mjini Kharthoum kwenye mchuano wa marudiano wakuwania tiketi yakushiriki kombe la CHAN 2014 nchini South africa ( Burundi 1 - 1 Sudan).

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire