Mchuano wa marudio na wa mwisho kwa upande wakinyanganyiro cha kombe la CHAN ulichezeka jana usiku kati ya Sudan mbele ya Washabiki wake kuipokea Burundi ,ifahamike ya kuwa Burundi kwenye mchuano wa awali ililazimika kwenda sare na Sudan Mjini Bujumbura bao 1-1. Kwenye mchuano wa jana orodha ya Wachezaji waliotangulia ni ile tulio ichapa kuwa ya weza kuanza mchuano huo apo kabla. ( Arthur,Kaze Gilbert,Issa Vidic,Rashid Léon,Lule,Gael,Lucio,Papa Claude,Celestin na Tambwe Amissi). Kipindi cha pili palikuwepo mabadiliko Célestin Abasi Habonimana alimpisha Shabani Hussein Tchabalala , fasi ya Nahimana Papa Claude ikachukuliwa na Aime Nzohabonayo. Dakika 45 za kipindi cha kwanza kilimalizika Burundi ikiwa imeshafungwa bao 1kwa 0. Walipotoka mapumzikoni wa Coach wawili NASSIM LOFTY na AMARS NIYONKURU walibadili mkenyuro na mambo hayakukawia kwani kijana Kaze Gilbert Demunga ali isawazishia timu yake kwenye dakika ya 50 ya mchezo huo . Palikuwepo kosa kosa pande zote mbili ila Kipa wa Burundi Arakaza Mc Arthur alikua ekenge hakuna bao hata moja lililopatikana pande zote mbili. Dakika 90 kumalizika , Referee wa mchuano huo kwa ushirikiano na wenzie wakawa wameamuwa wapige manati ya penalti. Wachezaji wa Burundi waliopiga ni pamoja na Gael , Aimé nzohabonayo,Christophe Nduwarugira Lucio,Demunga walifunga kinyume na Tambwe Amissi pekee yake ndie alieshindwa . Kwa upande wa Sudan,wachezaji wawili walimpa mpira Kipa wa burundi Mc Arthur ambae ilikuwa ni siku yake kweli (Jumla ya 4-2) . Duru kutoka Sudan kwa Mtangazaji ACHEL zinasema kuwa Tambwe Amissi yawezekana kutoshirikiana na wenzio kwani atapita anaendelea Saudia Arabia kuyafanya makubaliano na timu moja wapo ya pande zile,na waki afikiana moja kwa moja timu hio lazima irudishe pesa kwa timu ya Simba kutokea Tanzania ambayo ilikuwa tayari ilishampa mkataba wa miaka 2 . Kombaini hiyo ilio iletea heshma nchi yetu inasemekana kuwa itarudi nchini mnamo saa sita usiku (Minuit) kwani watatoka Khartoum saa nane mchana (14h). Tayari Burundi imejiorodhesha kwenye kitabu cha heshma cha Africa , historia iliandikwa jana saa tano usiku ,hongera sana kwa kila mtu aliechangia kwakusema tufike kwenye atuwa hio muhimu sana . Mashindano hayo yamepangwa kufanyika ifikapo tarehe 1/January/2014 - 1/February/2014 nchini South africa kwa Madiba Mandela .
* Primus League iliendelea mwishoni mwa jumaa , matokeo :
Ijumaa 26/07/2013Ligue B Bujumbura: Saa tisa: Umoja 1 - 4 Messager Bujumbura
Jumaa-mosi 27/07/2013
Ligue A: Saa kumi : Prince Louis 0 - 3 Flamengo
Jumaa-pili 28/07/2013
Ligue B Bujumbura: Saa nane: AC Tanganyika 0 - 3 Les Guêpiers du Lac.
Ligue A: Saa kumi : Académie Tchité 2 - 2 Royal . Mwishoni mwa Jumaa ligi inaendelea...
Jumaa-mosi 27/07/2013
Ligue A: Saa kumi : Prince Louis 0 - 3 Flamengo
Jumaa-pili 28/07/2013
Ligue B Bujumbura: Saa nane: AC Tanganyika 0 - 3 Les Guêpiers du Lac.
Ligue A: Saa kumi : Académie Tchité 2 - 2 Royal . Mwishoni mwa Jumaa ligi inaendelea...
Unité Fc kwenye uwanja wa Mukoni /Muyinga |
Fahamu vizuri : Timu ya Unité/Muyinga ilifunga Olympic Star ,moja kwa moja imejikatia tiketi yakuchuana na Volontaire kwenye fainali,mshindi ndie atapanda daraja la kwanza kwa upande wa Ligue B Mikoani.
Msimamo wa Ligi :
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire