mardi 16 avril 2013

Exclusive : Jokate na Penny wanazungumzia uhusiano wa kimapenzi wa Diamond na Irene Uwoya ...


Katika muda ambao kila mmoja alikuwa amejaribu kuamini kuwa Diamond Platnumz ameamuwa kutulia na mpenzi mmoja . Mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa hivi karibuni kumezuka tetesi kuwa Staa huo wa 'Ukimuona' ,ameanzisha uhusiano wakimapenzi na muigizaji wa filamu Irene Uwoya . Baadhi ya magazeti ya udaku nchini tanzania yameandika habari hio ikiwa na picha inazowaonyesha mastaa hao wakichukuwa chumba kwenye hoteli ambako yalidai walienda kufanya yao.
Kwa upande wa mpenzi wake wa zamani JOKATE Mwegelo alikanusha habari zilizo andikwa kuwa yeye alimcheka Irene kwakunaswa kwenye himaya ya Diamond ,alisema kuwa hayamuhusu na ahitaji azungumzwe kwenye habari hio . Kwa upande wa Penny mpenzi wasasa wa Diamond , alisema kuwa :"Wameshayazungumza ,mimi na Diamond tuko zetu vizuri , sipendi kuzungumza mengi ."

1 commentaire: