samedi 2 mars 2013

Miss Bikiyo :" Ibitakuraba uraba hasi..."( Kazi mbele,maneno baadae)



GIRUKWISHAKA Fidelite KEZA a.k.a Miss Bikiyo,a.k.a Miss G-Flo Mzaliwa wa MUKIKE Jijini Bujumbura Vijijini (Bujumbura Rural) nchini Burundi tarehe 2/December/1991 , mtoto wa 4 kati ya wa 6 waliozaliwa toka kwenye nguvu za wazazi wake wawili NGENDAKUMANA Leon na HABONIMANA Leocadie ambao wote walisha ondoka dunia toka mwaka 2005 . BIKIYO ni Msanii kati ya Wasanii wa kike ambao wanafanya vyema nchini kwa upande wakuipeperusha bendera nje na ndani ya nchi kupitia nyimbo kadhaa na video zenye mvuto na zenye gharama ya hali ya juu . Msanii huo ambae kipindi cha nyuma alikuwa nje ya nchi kufwatilia nyimbo zake za album ambayo ataiyachiya hivi karibuni alichukuwa fursa yakuandika kwakuomba msamaha na kuomba raia wajitume kufanya kazi bila kujali maneno yanayo semwa huku na kule . Huu ni ujumbe alio uwandika kwenye ukurasa wake wa facebook Msanii wa kike Mrundi GIRUKWISHAKA Fidelite a.k.a Miss BIKIYO baada ya Washabiki wake wasiokuwa wadogo kumlaamu kuwa wanamuandikia ujumbe kwenye ukurasa wake wa facebook ( inbox ) kisha hawajibu , ali andika : "Hello Friends and Fans nkaba banje gusaba imbabazi kubantu bose banyandikiye Inbox ntashoboye kwishure nari mfatiriwe n'ibikorwa vyinshi nkuko mubizi ko ndiko ndakora album , album nayo isaba kuba uri posé fcbk hariho igihe isamaza , Ibikorwa ndimwo ubu ndabikesha ino Video Serious man , Uyu n'umwanya wo kugwiza ibikorwa vyiza no bla bla ........ Mugenzi fata umwanya wogukora akazi kiwawe apana kuja gufukura uvuga ibintu bitakuraba , ndashimira aba fans banje mukwakira neza video yanje SERIOUS MAN ikaba ubu inshakanye ahantu ntari niteze , Don't juge aaaah this is my style Serious Man , I like it.Thx ALLAH " . Tukizingatia ujumbe huo kwa kina Msanii huo anaomba watu msamaa kuona anakuwa anakawiya kuwajibu wanapo muandikiya,ilo ni jambo la busara na laubinaadamu kwani wasanii wengi huwa hawakumbuki kuwa bila mashabiki , wao hawawezi kuwepo kisha aliomba watu waache roho za kwanini,kazi mbele kisha maneno baadae anahimiza raia watumike na waache kutizama vyawengine , na hio ndio siri yamaendeleo...Alimshkuru mungu kuona amepiga hatuwa japo sio jambo rahisi kuweka album yenye ufundi wa hali ya juu hewani bila kukutana na mitihani tofauti tofauti huku na kule,ila yeye anasema kuwa hajali na kwa upande mungine inampa nguvu zaidi yakuendelea .Twamtakia kheri...





Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire