Tamasha kabambi iliokuwa imenadiwa kuwa ndio kutangaza hadharani kundi lao jipya la 'MACHIRUKU' kwa vijana wawili Franck BUKURU kutoka kwenye kundi la Wanajeshi kamili na Marechal Slai Fyiroko kutoka kwenye kundi la Wakali Power haikufanyika leo kama ilivyokuwa imetangazwa kupitia vituo mbali mbali vya upashaji habari ,vijiwe na sehemu mbali mbali kutokana na matayarisho na ukosefu wa pesa kwa waliokuwa walijikubalisha kuwa watajishughulisha na swali nzima la ufundi (Technique) . Alitwambia mmoja kati ya Wasanii waliokuwepo kwenye bango :" Concert haitofanyika tena ,na tumeanza kuwapigia sim wengine waimbaji wasiwasili , ni kuwa tumepata tatizo yakiufundi tulikuwa tumeskilizana na mwenye anajiusisha na ufundi kuwa tutamlipa baada ya Concert ila hakutaka kutuamini na ndio maana tumeamuwa kuachana nayo,twaomba radhi watu wote ambao walikuwa tayari kwakuja kutupa sapoti." Hali kama hii ya Concert kuhomba itaisha lini Burundi jamani ?
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire