MAMA wa Wema Sepetu, Mariam Sepetu juzikati alitoa kali ya mwaka baada ya kumvaa Dj na kutaka kumchapa vibao kisa kikiwa ni kupiga nyimbo za aliyekuwa ‘mkwe’ wake, Nasib Abdul ‘Diamond’.
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni nyumbani kwa Mtangazaji wa Clouds TV na Redio, Zamaradi Mketema, Mbezi Beach jijini Dar kulikokuwa na ‘bethidei’ ya mwanaye aitwaye Russel.
Wakati watu wakiendelea kuburudika, Dj aliweka wimbo wa Diamond wa Nimpende Nani ambapo ghafla mama Wema alionekana kuhamaki pale wimbo huo ulipofikia ile sehemu inayosema: ‘Usiwe kama Wema Sepetu, kila siku magazeti’.
Mara mama huyo akiwa amefura aliinuka na kwenda kwenye meza ya muziki na kuuzima kisha ‘kumuanzishia’ Dj huku akimchimba mkwara kuwa hataki kusikia nyimbo za Diamond popote pale anapokuwepo. “Hivi wewe Dj toka nifike ni nyimbo za Diamond, hakuna nyimbo nyingine? Nakuomba sehemu yoyote utakayoniona mimi usiweke nyimbo hizo, sawa… na hivi sasa badili wimbo,” alisikika mama huyo akisema kwa hasira.
Kufuatia mkwara aliochimba mama huyo, Dj alikuwa mpole hivyo kuachana na nyimbo za Diamond na kupiga nyingine ili kuepusha shari.
SOURCE: globalpublishers
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire