samedi 16 février 2013

Norway: -FEMI DE JABAT :" Kora ndabe iruta vuga numve." (Nina mipango mingi kwa nchi yangu Burundi ila sijapenda kuiweka hadharani).


NSENGIYUMVA MINANI FELICIEN alias Femi De Jabat mwanamuziki Mrundi anae ishi nchini Norway blog yetu hii imechukuwa nafasi nyeti yakufanya mahojiano nae kuhusikana maisha anayoishi pande zile na mipango anayo kama raia wa Burundi. Ebu soma maswali tuliomu uliza na majibu aliotujibu ,tulianza kumsali "Habari yako Mzee?",akatujibu :

Femi : Safi kabisa,ila bado sijawa Mzee samahani...

AH : Aahhhhaaa...siunajuwa tena heshma kwa anae kushinda na unaemshinda miaka ni muhimu?

Femi : Aaahhaa....yeah! nilikuwa nakutania tu! Siunajuwa tena watu wengi hawapendi unakapo wambia kama wameshakuwa Wazee.

AH : Kweli,ila endapo Mungu atatuazima pumzi hali iyo itatufkia sote. Vipi uko binaendeka? Maisha ya kila siku,muziki vipi unajipa kweli uko?

Femi : Kwa ujumla niko vizuri na familia yangu , Mungu anasaidia . Kazi za kila siku ni sawa kwani inaendelesha familia,kwa upande wa muziki kwa kweli siwezi sema kama unaweza kuendelesha maisha yangu hapa,unaona sisi siwazaliwa wa hapa inatuweya ngumu sana,huwa naingia Studio nakapokuwa likizo la sivyo niwakati nainapopata muda wakutosha kabisa.

AH : Yani muziki uko umesimamisha?

Femi : Duuh! Inaweza kuwa ngumu kusimamisha kwani biko mu damu naninapenda sana muziki,niko najipanga hivi karibuni tutowe nyimbo na binti wangu NDIHOKUBWAYO MUGISHA DIVINE ana miaka 16 (16 ans) , kwa muda huu yuko anajifunza Guitar. Niko namsaidia ili hivi karibuni arikodi nyimbo yake ya kwanza . Nimepanga airikodie Lydhagen Studio ni ya hapa hapa NORWAY, Producer anajulikana kwa jina la TONY WADE . Na ndio namimi nilitumika na nikaiweka hazarani album yangu ya 5 *MPORE BURUNDI*. 

AH : Kinyume na hio nyimbo unamipango ipi na nchi yako ?

Femi : Msiku za mbele nimepanga kuja kutembea nyumbani, niko na mpango mzuri sana na nchi yangu 'Burundi' ila ndugu yangu siunajuwa tena binaadamu afadhali ninyamanze nitakapo fika watu wataona nini nitakacho kifanya,wazee wazamani ndio walisema 'Kora ndabe iruta vuga numve' ,sasa wait and see.

AH : Nakushkuru sana na Mungu awabariki kwenye shughuli zenu za kila siku.

Femi : Mimi njo nazitowa shukran kwako ndugu,Mungu akubariki...

AH : Asante...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire