|
Juliana Kanyomozi. |
Juliana Kanyomozi, Diva wa muziki kutoka nchini Uganda, Ijumaa hii anatarajiwa kuandika historia ya kipekee katika tasnia ya burudani kwa kupitia onyesho lake kubwa la muziki ambalo limepatiwa jina Upclose And Personal With Juliana” Onyesho hili ambalo litafanyika huko Uganda, linafanyika pia kwa manufaa kwa jamii kutokana na waratibu kuweka wazi kuwa sehemu ya mapato yake yatatumika katika shughuli ya hisani, kusaidia shule ya sekondari ya wasichana ambayo inafahamika kwa jina Terpu ya huko huko nchini Uganda .
Kiingilio katika onyesho hili kimetangazwaMwanadada kuwa ni kiasi cha shilingi 100,000 za Uganda, na kwa mujibu wa waratibu, mpaka sasa kila kitu kinakwenda katika mstari tayari kwa Juliana kufanya yake jukwaani siku ya Ijumaa.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire