samedi 18 janvier 2014

RONALDO KUWANUNULIA GARI JIPYAA MADAKTARI REAL MADRID BAADA YAKUNYAKUWA BALLON D'OR 2013


Ni kazi ngumu kuwa mchua misuli wa Cristiano Ronaldo, lakini wakati mwingine inalipa.
Mchezaji huyo ambaye hivi karibuni ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, FIFA Ballon d’Or amewaahidi madaktari wa Madrid kuwanunulia gari mpya baada ya kushinda tuzo hiyo wiki hii .
Katika mahojiano ya hivi karibuni na Sportsmail, kocha wa Real Madrid , Paul Clement amezungumzia mambo ambayo Ronaldo atayafanya atakaporejea kutoka kwenye mechi za katikati ya wiki za Ligi ya Mabingwa . Ronaldo anatambua na kuheshimu sana mchango wa madaktari wake na wakati wote amekuwa mkweli wa ahadi kwao na awali amekwishawahi kuwazawadia saa mpya na simu aina ya iPhones toleo jipya.

All in! Ronaldo was pictured having a massage with the Madrid medical team last month

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire