mercredi 17 avril 2013

SUDAN : Wachezaji wa kigeni wa El Mereikh wanamaliza miezi 4 bila kupewa marupurupu (Salaire)...
Duru kutoka Jijini Karthoum nchini Sudan zinasema kuwa wachezaji wakigeni kwenye timu ya El mereikh wako kwenye hali mbaya na isioridhisha baada ya kutopewa mshahara wao takribani miezi mitatu na mwezi huu utakapo malizika watakuwa wametimiza miezi 4 bila kupewa marupurupu yao . Hali hio imeanza kuleta uhasama hadi mdaa huu kati ya Wachezaji vigogo ambao baadhi wameanza kuihama klabu hio nakurudi manyumbani nikizungumzia kipa mkongwe Hicham El Hadary (Misri) ambae aliamuwa kurudi nyumbani nakutishia kutorudi hadi atakapo lipwa pesa zake . Mungine ni kutokea Ivory Coast . Wengine wachezaji akiwemo Mchezaji wakimataifa kutoka Burundi Yameen Selemani NDIKUMANA tayari wamenyanganywa vitambulisho vyao ili wasisubutu kutowa siri hio kwenye nchi zao ili timu hio baadae ije kuchukuliwa hatuwa na Shirikisho la dimba barani africa CAF kulinganisha na sheria ya kuwalinda na kuwapa huduma chini ya msingi wa makubaliano walio yasaini kabla mchezaji anapoitika kujiunga na timu yeyote (Contrat) .


Hali hio ilikuwa ngumu hadi kufkia Wachezaji hao kugoma kucheza mchuano wa duru ya marudiano (Match retour) walipo pambana na klabu kutokea Angola nakusababisha kupigwa nakuondolewa mashindanoni . Kinyume na Wachezaji hao ambao wamesha anza kurudi makwao , Selemani Yameen tulipo mu uliza baada yakupata habari hii kupitia moja kati ya majarida (gazeti) nchini pale.


Alitusimulia kuwa :" Nimeshanyanganywa kitambulisho changu , alakuli hali endapo mwezi huu hawakutupa marupurupu yetu nina imani kusitisha mkataba nirudi nyumbani kwani nilishavumilia sana , huu ujumbe ni kwa niaba ya washabiki wangu isije kutokea kisha wapokeye vingine ."


Kwa kirundi : (Bamaze kunyaka Passport yanje,uko bizogenda kwose batampaye amahera yanje kumwisho wukukwezi ntankeka ko nzoca mpagarika contrat twari twasinyinaranye ,ndabivuze uko kubwa basanzwe banshigikira (Fans) babimenye hakiri kare ). "

Blog yako inaendelea na uchunguzi wa kina,akipenda Mungu tutakujuzeni hali kadri inavyoendelea ...Ikumbkwe ya kwamba Yameen ni mmoja kati ya Wachezaji kitegemeo wa timu hio kulinganisha na mchango mkubwa anao utowa kwa upande waushambuliaji ,ni faraja kwa nchi yetu kuwa na kiungo hicho bora kinacho jivunia...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire