samedi 18 janvier 2014

CHAN 2014 : YAMIN SELEMANI NDIKUMANA aipa matumaini Burundi kuingia Robo fainali...

Pichani : Yamin Selemani 

Burundi imeyapata matumaini yakuendeleya kucheza ngazi ya robo fainali baada yakuandika alama 4 leo kwenye mchuano iliyomenyana na mauritania . Nchi ya Mauritania ilipata na fasi yakuandikisha bao la kwanza kwenye sekunde 54 , ila vijana wa Nasseem Lofty hawakuchoka walifanya kadri wawezavyo kupambana nakusawazisha bao hilo lilofungwa kwa kichwa na Abdul Razzak Fiston baada yakupata krosi nzuri kutoka kwa Yamin Selemani huyo huyo ambae alipata penalti kwenye dakika chache tuu na akawa amempa mlinda mlango wa Mauritania ambae alikuwa tayari japo kupoteza kwao alama tatu . kuzembea zembea kwa walizi wa Timu ya Intamba Murugamba kuliwasababishia kufungwa bao la pili... Burundi ikiwa yao ndio ilianza kupata bao la pili lililo fungwa na NDUWARUGIRA CHRISTOPHE alias Lucio baada yakutengenezewa vizuri na mchezaji mwenye kujituma na mwenye uchu wa ushindi Abdul Fiston . Burundi 2 , maurtania 2 . Palipo salia dakika 2 kwenye jumla ya 6 zilizo ongezwa na Refa kutoka Somalia Yamin Selemani NDIKUMANA mwenye umri wa miaka 24 ali ipa matumaini Burundi kuona robo fainali kwakupiga mkuki mlali nakugeuza ubao kwakuandika 3 kwa 2 kwa faida ya Burundi . Burundi itachuana na DRC Jumaa-tano huku Mauritania ambae imepoteza michuano miwili itakuwa ikipepetena na Gabon ambayo mapema leo imeikwamisha DRC kwa bao 1 kwa bila. ilikuwa ni nderemo na heko kwa raia wa Burundi pande zote ,furaha tele baada tu yakipenge kupulizwa mchezo kugonga ukuta .Pongezi kwaWachezaji wote waliyojituma kwa udi na ashabiki wote Warundi wanao zidi kuwapa sapoti Wachezaji wa Burundi ambao wanapeperusha bendera kwa Mandela .

Msimamo
1. Burundi 4 points
2 Gabon 4 points
3 DRC 3 points
4 Mauritania 0 point
Baadhi ya picha za Washabiki wa Burundi nje na ndani ya uwanjani leo :

 Kila la kheri kwa Vijana wetu ...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire