dimanche 10 février 2013

CAN 2013 : Nigeria bingwa wa Kombe la 29 la Mataifa barani Africa...



Nchi ya Nigeria imetwaa ubingwa wa mashindano ya Africa nchini Africa yakusini usiku wa leo. Mchuano uo umemalizika kwa bao 1 kwa bila,bao lilofungwa na SUNDAY Mba kwenye dakika ya 40. Match ilikuwa na mvuto wa hali ya juu tukilinganisha na fasi timu zote mbili zilipata,imekuwa tunzo la tatu Nigeria kujinyakulia , vile vile katika historia Stephen Keshy kutwaa kombe hilo kama Mchezaji na mwaka huu kama Coach. Mashindano yatakayofwata itakuwa mwaka 2015 nchini Maroc akipenda Mungu...

Jana Mali ilichukuwa na fasi ya tatu baada yakuilaza Ghana kwa bao 3-1.Mali ilipata goli la kuongoza katika kipindi cha kwanza katika dakika ya 21 likifungwa na Mahamadou. Hadi mapumziko Mali ilikuwa ikiongoza kwa hilo goli.Kipindi cha pili kilianza kwa Mali tena kufunga katika dakika ya 48, mfungaji akiwa ni Seydou Keita. Ghana ilijitutumua na kupata bao la kufutia machozi katika kipindi hicho cha pili. Hata hivyo furaha yao haikudumu sana baada ya kuchapwa goli lingine la tatu na la ushindi kwa Mali.Matokeo haya yanaendeleza ubabe wa Mali dhidi ya Ghana, ambapo mwaka jana katika mchezo kama huo wa kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika 2012, Mali iliichapa Ghana 2-0.
Ni mwaka mmoja kamili, wakati Ghana na Mali zilipokuwa zikijiandaa kucheza mechi ya kusaka nafasi ya tatu baada ya timu zote mbili kupoteza matumaini ya ubingwa zilipotolewa katika nusu fainali za michuano ya kombe la Afrika za mwaka 2012.
Ghana na Mali baada ya kukosa kombe hili, jitihada zinaelekezwa katika kutafuta nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 zitakazofanyika nchini Brazil.


















Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire