jeudi 21 février 2013

KIDUM :" I love so much my Mother..."

Msanii wakimataifa Mrundi ambae azidi kutikisa dunia kwa tamasha anazo zidi kuendesha pande zote  kupitia ujuzi na utajiri wa mashahiri usio chagua kuburudisha mzungu ao mweusi ameongea na safu yetu hii yakuelimishana nakuweka wazi kuwa :" Kama kuna mtu ninaye mpenda na ninae muheshimu zaidi dunia kuliko kitu chochote ni mama yangu mzazi , alie niweka tumboni miezi tisa , alie nivumilia kwa usumbufu wangu nikiwa bado child ,alie nilea na leo hii kila kona nakapo pita napewa heshma kutokana na malezi mazuri alio yanipa toka ningali mdogo hadi mdaa huu , ningeliwaomba jameni tueshimu wazazi wetu kwani bila wao sisi leo tungelikuwa wanani?". Ifahamike ya kuwa Mama yake mzazi bado angali hai na anaishi Bujumbura , Tarafani Kinama alipozaliwa Jean -Pierre NIMBONA KIDUM ambae ifikapo tarehe 23/February atakuwa Rwanda kwenye maonyesho ya FESPAD , na hivi karibuni anamulika kutembelea nchi za Africa ya kusini kama Swaziland nazinginezo kwenye Tamasha mbali mbali,kumbuka ya kwa mara nyingine tena KIDUM ndie anae shikilia tunzo la  'KORA AWARDS 2012'  kwa upande wa Best Male Artist in East africa of The year ,kwenye  mashindano yaliofanyika nchini Ivory Coast. Blog yenu inawa ahidi kuzidisha kuwapa picha za wazazi wengine wa Wasanii wa Burundi . Wait and see...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire