jeudi 26 septembre 2013

Vodacom League :BEKI LA NGUVU KAZE GILBERT NA MSHAMBULIAJI HATARI TAMBWE WAREJEA KAZINI SIMBA SC

Tambwe Amissi na Demunga
BEKI Kaze Gilbert aliyeumia nyonga Jumamosi Simba SC ikimenyana na Mbeya City na kutoka sare ya 2-2 katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, anatarajiwa kurejea mazozini leo baada ya kupona.
Aidha, Mrundi mwenzake Amisi Tambwe aliyeumia pia nyama katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, naye anatarajiwa kuanza mazoezi jana.
Kaze akipata matibabu ya kwanza.


Simba SC itashuka dimbani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumapili kumenyana na JKT Ruvu katika mfululizo wa ligi hiyo, wakati Rhino Rangers itamenyana na Kagera Sugar Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora, Mbeya City na Coastal Union Sokoine, Mbeya, Mgambo JKT na JKT Oljoro Mkwakwani, Tanga na Ashanti United na Mtibwa Sugar, Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam . Mechi nyingine itachezwa Jumamosi, Yanga SC na Ruvu Shootings Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati leo Rhino Rangers wanaikaribisha Ashanti United Mwinyi, Tabora.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire