samedi 5 octobre 2013

Bongo music News: Bifu ya Man Walter na 20% hatimaye yamalizika...

Kwenye ukurasa wa facebook wa Magic Fm na Channel Ten taarifa hii imetolewa hivi..

Hatimaye bifu kali kati ya msanii aliyewahi kutwaa tuzo 5 za KTMA nchini kwa pamoja na kuvunja rekodi, TWENTY PERCENT na aliyewahi kuwa Producer wake pia mshindi wa tuzo ya matayarishaji bora wa muziki nchini KTMA 2012, MAN WATER, limemalizika rasmi kwa wawili hao kukutana na kumaliza tofauti zao.

Man Water na Twenty Percent walikutana na wawili hao wamekubaliana kufanya kazi tena pamoja na kusahau yaliyopita.

Akizungumza kiundani kuhusu tofauti zao Man Water alisema tatizo lilikua ni kutoelewana au kupishana kwa kauli ambazo walizimaliza na hatimaye kuweka mikakati mipya ikiwemo ya kufanya kazi pamoja kwa makubaliano maalumu.

Kwa upande wake 20% amesema tofauti zao hazikuwa za msingi bali ni kupishana tu kwa kauli na sasa yuko tayari kufanya kazi pamoja na Man Water.
Inaaminika kwamba kufanya kazi pamoja kwa wawili hao kunaleta mwamko mkubwa kwa washabiki wao kutokana na kuelewana katika kazi zao mbalimbali walizowahi kufanya ikiwemo kaziya Yanini malumbano, Tamaambaya, Mama Neema na nyinginezo.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire