mercredi 18 septembre 2013

CHAN 2014 : Burundi,Gabon,Mauritani na DRC kundi moja,Tambwe Amissi atikisa wavu mara nne leo hii...


- Burundi imepangwa kwenye kundi D ,itachuana na Mauritania, Gabon na DRC . Makundi yote yamepangwa ifwatavyo :

Group A:
South Africa
Mozambique
Nigeria
Mali

Group B:
Zimbabwe
Morocco
Burkina Faso
Uganda

Group C:
Ghana
Congo-Brazzaville
Ethiopia
Libya

Group D:
DR Congo
Mauritania
Burundi
Gabon
                                  Vodacom League Tanzania :


- SIMBA ya Dar es Salaam leo imedhihirisha umwamba wake mbele ya Mgambo Shooting inayomilikiwa na JKT kwa kuicharaza mikwaju 6 -0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.


Magoli ya Simba yaliyo fungwa na Amisi Tambwe magoli 4 na Haruna Chanongo goli 2 yameiwezesha Simba kushika usukani wa Ligi ambayo ilikuwa ikiongozwa na makanda wengine wa JKT Ruvu ambao leo wamecharazwa mjeledi 1 na raia wa Ruvu, Ruvu Shooting.

Wakati Simba ikishangilia karamu hiyo ya Magoli imekuwa ni Mwimba kwa mahasimu wao ambao pia ni mabingwa wa Soka la Tanzania Yanga juma lililopita walitimuliwa kwa mawe na watoto wa Mbeya Mjini, Mbeya City kwa sare ya 1-1 na kukimbilia katika gereza la Mbeya ambako Askari wa Magereza timu ya Prisons ya Mbeya nao kuwaavua kandambili na kutoka sare 1-1.


Wazee wa Lambalamba watoto wa Chamazi Azam FC nao wamepigwa jua na kuyeyushwa na watoto wa mjini Ashanti United kwa sare ya 1-1.

Huko Kwa wakata Miwa wa Kagera, ndani ya Kaitaba Bukoba, Kagera Sugar nao wamelazimishwa suluhu na Wajeshi wa Arusha JKT Oljoro.

Mchezo mwigine ulio shuhudia sare ni ni Ule wa Wakata Miwa wa Turiani Mtibwa Suger iliyo toka sare ya bila kufungana na watoto wa Mbeya City.


Wagosi wa Kaya Coastal Union ya Tanga nayo imekutana na Wajeshi kutoka Tabora, Rhino Rangers na kutoka sare ya 1-1 wakiwa Mkwakwani.

Fahamu vile vile ya kuwa Tambwe aliyetokea Vital’O ya Burundi alifunga mabao manne leo katika dakika za nne, 41, 44 na 76 kwa penalti, baada ya beki Bashiru Chanache wa Mgambo kuunawa mpira kwenye eneo la hatari, wakati Haroun Chanongo alifunga mawili pia dakika ya 32 na 64.
Kwa ujumla Simba SC iliwapa raha mashabiki wake leo kwa soka safi na ushindi mnono.


Waliocheza Simba SC leo : Abbel Dhaira, Miraj Adam/William Lucian ‘Gallas’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Kaze Gilbert, Joseph Owino, Jonas Mkude, Amri Kimeba, Henry Joseph/Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Betram Mombeki, Amisi Tambwe na Haroun Chanongo.

Msimamo wa ligi:-

1. Simba .... 4 . 9 .. 10
2. JKT Ruvu 4 . 5 .. 9
3. R Shutin. 4 . 4 .. 9
4. Yanga .... 4 . 4 .. 6
5. Azam ..... 4 . 2 .. 6
6. Coast ..... 4 . 2 .. 6
7. M. City .. 4 . 1 .. 6
8. Kagera .. 4 . 0 .. 5
9. Mtibwa . 4. -1 .. 5
10. Mgambo 4 -8. 3
11. Rhino .. 4. -2 .. 3
12. Prisons. 4. -6 .. 2
13. Oljoro.. 4. -4 .. 1
14. Ashanti 4. -7 .. 1

Wafungaji bora :

Amissi TambweSimba SC4
Haroun ChanongoSimba SC3
Jerry TegeteYanga SC3
Jonas MkudeSimba SC2
Didier KavumbanguYanga SC2


Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire