Habari zinazo zidi kugonga vichwa vya habari na kwenye baadhi ya mitandao nchini Tanzania ni kuwa hapo jana tarehe 18/Sept/2013 mastaa wa filamu Chuchu Hans na Blandina Chagula(Johari) wamefumaniana kisa ni muigizaji mwenzao Vicent Kigosi(Ray).
Inadaiwa kuwa Johari ndiye amemfumania Chuchu nyumbani kwa Ray maeneo ya Sinza, Dar es salaam na wawili hao kuanza kufumuana makonde na baadaye Ray kuwahi kuwaamulia kabla mambo hayajaharibika zaidi.
Habari za chumbani zinaarifu kuwa Johari na Ray ni wapenzi lakini kwa muda mrefu wamekuwa wakijificha kukwepa kuanikwa magazetini. Siku za nyuma Ray alipokuwa ulizwa swali hilo kupitia kipindi *Mkasi* cha SALAMA alikana nakuashiria kuwa hana uhusiano wowote na Johari bali tu wanapokutania ni kuongoza kampuni wanayochangia 'RJ Company' . BB inakuahidi kufwatilia kwa karibu habari hiyo , pengine ikawa skendo ila tunaendelea na uchunguzi wa kina...
Huu apa ni ujio mpia wa RJ Company
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire