lundi 23 septembre 2013

ALIDA Nyota itakayo nga'ara msikuu za usoni kwa upande wa mziki kanda nzima ya Africa mashariki...

Photo : Sat-b Satllight , me , Washington and rap nature at Casablanca .
Pichani wakiwa UGANDA na Washington

Tarehe 20/September/2013 sehemu pajulikanapo kama * Cafe Bambou * ndipo Mwanadada ALIDA BARANYIZIGIYE alipokusanya watangazaji na waandishi wa habari kwa kuwaeleza mengi kuhusu yeye nakuweka bayana kazi yake ya mziki. Ali itisha mkutano huyo siku mbili kabla yakurejeya nchini Rwanda anapofanyiya kazi na mdaa mwingi huwa anakuwa yupo kule . ALIDA kwenye mkutano huyo alitufahamisha kuwa : « Mimi ni mwanamuziki mwanye asili ya Burundi ,nimezaliwa Bujumbura ,nipo kwenye game ya mziki yapata sasa miaka 12 ,nilianza kama Msani wa injili niki imbiya kwenye kanisa la Vivante tarafani Jabe/Bwiza : Baada ya hapo niliungana na makundi tofauti tofauti ya ya live Band kabla yakujielekeza Mjini Kigali ambapo nafanyiya kazi kwasasa .Siku zilizopita nilipata fursa yakuitishwa na kampuni ya Brarudi kuja kutowa mchango wango kwakuchakachuwa wasanii ambao walikuwa mashindanoni ,kazi niliyo ifanya bila pengamizi na maenzi ninayo yakuindeleza nchi yangu kwa upande wa mziki . Kumalizika kwa mashindano hayo kumenipa nguvu ingine yakutumika kwa udi na uvumba alakuli hali nione kuwa nimetambulika sana nchini mwangu na nyimbo zangu kuzikonga nyoyo za wapenzi wa mziki , na ndio kwa maana hiyo ninaichukuwa fursa hii kuwafahamisha kuwa narejeya kwa mara ingine tena kwenye game ya mziki kwa hari na nguvu nyingi . Kiukweli mdaa ukiwadiya huwa unabijiskiya na nio kwa maana nimeamuwa kuwakutanisha ili ujumbe huu mu ufikishe mbali . » Ifahamike ya kuwa ALIDA ni msanii ambae anajichanganya na mitindo mbali mbali ya mziki kama Jazz,blues,dancehall,reggae,afro music na mitindo ya zouk ,mwenye alitufahamisha kuwa habaguwi hachaguwi ,na huwa mara zote yupo tayari kufurahisha raia kati ya miaka 7 hadi 77,na huwa anajiskiya huru sana anapopiga live kuliko play back . ALIDA ni mmoja kati ya wasanii wakike wanao imba na ndioyo kwa maana hiyo ameamuwa kujikwamuwa vyakutosha ili awe chombo muhimu kwakuitambulisha zaidi nchi yake kwenye maziwa makuu,barani hadi nchi za mbali . ALIDA ni msanii anaye tumiya lugha mbali mbali kama kirundi,kifaransa,kingerea,kinyarwanda ilimradi ujumbe wake ufike kwa walengwa na yupo tayari kuzifanya kolabo na wasanii wenye ujuzi kwenye kanda ya  africa mashariki (East africa) na atimaye Burundi kama hivi karibuni nyimbo aliyo ifanya na BIZIMANA ABOUBAKR KARUME a.k.a Sat b Simba imeshakwisha ila hawakufurahishwa na production ya Washington The Magic nchini Uganda,wanamulika kufanya marekebisho kidogo kisha iruhusiwe kuchezwa kwenye redio tofauti . Clip video na audio walibitengenezeya nchini Uganda na hivi karibuni video hiyo itaanza kuonekana kwa baadhi ya runinga za kanda hii . Pini hiyo inaitwa *Stay with me *. ALIDA amekuwa msanii wa tatu baada ya Sat b , Wafaransa ndio wanasema « La charité bien ordonnée commence par soi-même » , akimaanisha kwa kiswahili « Zawadi nzuri kila siku inaanziya nyumbani » na ndio kwa maana alianza kukutana na médias ili afkishe ujumbe wake na wao watumiye fursa hiyo ili kutangaza ujumbe huo. ALIDA alimalizia nakusema : « Niliona umuhimu wa watangazaji kwenye mashindano yaliyo malizika ya PRIMUS nikasema nikiwa nawo mipango yangu yaweza kufika mbali sana na ndio kwa maana leo hii nimewakusanya. »
Alida akiwa na Kiongozi wa Jury, Buddy Magloire.


- Fahamu ya kuwa ALIDA yupo na nyimbo 8 zake binafsi , alishatumika kwenye Studio kubwa kubwa barani Africa kama :

Narrow road Production pamoja na PASTOR P Mjini Kigali , alifanya naye kazi 5 :

-Bizorangira

-Let it go

-I feel alright

-Liberte (Zouk)

-Let me love you ,kolabo na ALFA mshindi wa Tusker Project Fame.

-Nguma iruhande,nilitengenezeya *Next Level Records * Studio ya Bujumbura inayomilikiwa na  Buddy Magloire . Pastor P alipokuwa dhiarani Burundi alitumiya studio hiyo , ila malipo yote nilikuwa nimeyafanyiya Kigali kwenye Studio yake.
Alida


* Tanganyika Studio :

-Ngwino hano feat BACHIR DIA ,ambae aliumiya lugha ya ki wollof ya kwao SENAGAL.



* Next Level Records
· -Ndagukunda alitengenezewa na AMIR PRO, pini hiyo inatamba sana kwenye Redio tofauti tofauti za hapa nchini na tayari kuingiya kwenye top ten za baadhi ya vipindi.

· Lakufahamu lingine nikuwa ALIDA yuko mbiyoni kurodi pini na Big Fizzo , hayo aliyatufahamisha tulipokuwa kwenye kipindi live na Fizzo mwenyewe kupitiya 88.2 na 99.9 Mhz Culture Radio . Alitwambiya :” Fizzo namkubali sana , anaweza na ndiyo maana nimemuomba tufanye naye kazi akawa amenikubaliya , siku itakapo wadiya kitu kitawekwa hewani. “

« Niliona umuhimu wa watangazaji kwenye mashindano yaliyo malizika ya PRIMUS nikasema nikiwa nawo mipango yangu yaweza kufika mbali sana na ndio kwa maana leo hii nimewakusanya. » BB inamtakiya mafahanikiyo mema…

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire