dimanche 26 mai 2013

Djibouti : NZOKIRA JEFF ateuliwa Kipa bora baada ya timu yake A S A S DJIBOUTI TELECOM kuwa bingwa msimu huu...


Kipa wakimataifa Mrundi NZOKIRA Jeff maarufu KASEJA ambae anasakata gozi la kulipwa nchini Djibouti ameteuliwa kuwa Kipa bora baada ya Ligi kugonga ukuta huku timu yake ASAS DJIBOUTI TELECOM kufunga bao 6-0 kwenye mchuano wa mwisho walio ucheza Ijumaa . Jeff kati ya michuano 22 alio icheza bila kuwekwa kwenye akiba simbaya hata mchuano umoja alifungwa bao 9 pekee yake na hivo kumuweka na sawa na jopo la waandalizi wa Ligi hio kumteuwa rasmi kama Kipa bora wa Msimu huu . Jumla ya Timu 10 zikiwemo : A S A S DJIBOUTI TELECOM , DIKHIL, AS PORT ambayo itacheza CECAFA mwezi June , GEULLEH BATAL , AS C.D.E COLAS, TADJOURAH , S.I.D, GENDERKERIE , ARHIBA , EAD FC BALBALA ndizo zimediriki kwenye Ligi hio...

Ifahamike tu ya kwamba Timu yake hio itashiriki mwaka kesho michuano ya timu zinazokusanyika kwenye upande wawa arabu ( League Arabe ) ,na huku DIKHIL ilioshika na fasi ya pili kucheza CECAFA ya vilabu maarufu kama Kagame Cup mwaka kesho...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire