Mmoja kati ya Wasanii vigogo kutoka nchini Burundi Minani Nsengiyumva Felicien maarufu Marechal Femi De J’Abat ifikapo tarehe 25/June/2013 saa tisa unusu atakuwa amewasili nchini Burundi baada yakipindi kirefu akiwa anaendesha shughuli zake nchini NORWAY. Tulipo ongea nae alitufahamisha kuwa :" Nafarijika sana kuona ntarudi nchini mwangu na nia na madhumuni nikuja kuakikisha nimeiweka hadharani mipango niliojikubalisha ya maendeleo ya nchi yangu.Naleta msaada kwa kombaini ya Watwa wanao ishi pande za Bujumbura Vijijini kupitia Shirika la “VONECOVIC” linalo wasapoti kwa mipangilio yao toka mwaka 2007, shirika hilo linasimamiwa na Angela Iroegbu-Schauer." Ifahamike kuwa Femi De JAbat ndie muanzilishi na kwa mdaa huu ndie naibu wa Shirika hilo.
Lakufahamu vile vile ni kuwa msaada miaka ya nyuma waliwapa watwa hao mbuzi,kuku zakufuga,bidhaa za ndani,mahema,nguo navinginevyo . Femi aliongeza kutufahamisha kuwa ni fursa nyeti yakukumbuka raia hao walio sahaulika sana,wanao ishi maisha yakutombolesha. Kwa mwaka huu hawataweka mbali vifaa vya shulekuwatoto wa masomo,mnafahamu sana kuwa jamii hio hawasomi kama inavyoitajika nchini. Mwaka huu watateremka na bajeti ya pesa milioni 5 sarafu za burundi ili kuhakikisha mpango huo unafaanikisha.
Kwenye mipangilio anayoteremka kuindesha nchini nikuanzisha rasmi Shirika jipya la 'CERACIRE' “Cercle des Réssortissants et Amis de la Commune Isare Résidant à l’ Etranger”,ikiwa ni mkusanyiko wawarundi wazaliwa wa Tarafa ya Isare waishio nje ya nchi, shaba yake nikusongesha mbele Tarafa aliozaliwa. Ujio wake vile vile itakuwa ni fursa nyeti yakutengeneza picha (video) ya nyimbo * Shimira imana* ya Msichana wake NDIHOKUBWAYO MUGISHA DIVINE . Jopo nzima ya burundi beat inamtakia kila la kheri na fanaka kwa uzalendo anao wakusaka maendeleo nchini mwake. Komera kumuheto Marechal Femi De Jabat...
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire