Aisha Amuri NDIMUBANDI ,Mtangazaji Presenter anae pasha habari kupitia vibuyu vya anga vya Radio ya Umaa (R.P.A) ikiwa ni moja kati ya Radio zakibinafsi zinazoendelesha shughuli zao nchini Burundi. Mwanadada Aisha ambae anazoweleka sana kama mmoja ane jipa bidii kwakukuza nakuinuwa vipaji vya Wasanii wa hapa nchini na kanda nzima ya East africa kupitia kipindi chake maridadi 'East african music',alitufahamisha kuwa yuko na mpango unakao julikana kama *AISHA A GIVING FOR CHARITY* ikiwa ni mpango maalumu wakuitowa sapoti au msaada kwa watoto yatima. Alitwambia :" Tarehe 14/July ndio tarehe yakuzaliwa kwangu,ndugu zetu wengi wamezowea kwenye tarehe yakumbukumbu kuzaliwa kwao hua wanajumuika na ndugu,jamaa na marafiki kwa kushereherekea siku hio kwambwembwe nyingi ,ila mimi nimeamuwa siku hio nichangie na watoto yatima wa tarafani Kinama,ni sehemu mojawapo wanapo lelewa watoto hao." Aliendelea nakusema :" *AISHA A GIVING FOR CHARITY* ni mpango ambao umeshiba vilivyo, niliona mchango nitakao upata kupitia mikono ya wenye dola zao kama Mzee NJOVU HUSSEIN na hatimae mtoto wa Muheshimiwa raisi wa Tanzania JAKAYA KIKWETE ,mtoto anaitwa RIDHIWANI JAKAYA KIKWETE waliokubali kunipa shavu lazima nisinywishe watu togwa hadi wapagawe,kumbe nipanuke kichwa nanifikirie wale wasiojiweza hasa hasa mayatima." Alimalizia nakusema :" Ni fikra yangu,kwa yoyote ule atahitaji kujumuika nami itanifariji sana, nimeamuwa kuwa nafanya hivo kwa nguvu za Mungu kila mwaka ." Ikumbukwe kuwa ni Mtangazaji wa pili kuifanya sherehe yakuzaliwa kwake na kuitangaza kupitia vyombo vya habari kama alivyofanya hapo mwanzo Shani NKUNDABANYANKA alias Dj Ashanti mwaka uliopita, Dj Ashanti mwaka huo alijumuisha Watangazaji,Wasanii na Wadau wa mziki na ikawa fursa nyeti yakuchangia pamoja kwakupanuwana mawazo mbali mbali ili muziki wa Burundi upasuwe mbingu na ardhi usambae kote dunia. Habari ndio hio...
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire