vendredi 19 juillet 2013

Academie INTWARI imempokea Coach kutoka Holland ambae yuko ziarani Burundi kwa wiki moja...

Pichani: Abega,wachezaji na wakufunzi na vile vile Mgeni rasmi Van Marteen
Asubuhi ya leo tumeipata fursa yakuitembelea shule la mpira la vijana wasiozidi umri wa miaka 14 na 17,shule la mpira la Mh ABEGA mpenzi wa mpira mwenye shaba yakutaka kuendeleza nchi yake kwenye sekta hio. Nia na madhumuni yakudhuru kwenye shule hilo ilikuwa nikutizama wapi harakati zinapofikia kwa upande wausukaji watoto kwaniaba ya michuano yakimataifa barani na hadi ulaya endapo mikakati yakuzidisha mawasiliano na viongozi wa klabu tofauti tofauti pande za nje. Tulipofika tulikutana na Coach kutoka Holland anaetambulika kwa jina la  Peter Van Meerten akiwa ni Coach aliejitolea bila malipo kuja ku utowa mchango wake kwa timu hio ya vijana inayosadikiwa hadi mwaka 2017 kuwakilisha Burundi kwenye mashindano yakimataifa.
Pichani Coach Peter Van Marteen na watoto wa " Vision 2017 ".

Tulihojiana nae na akatueleza kuwa :" Niko Bujumbura kwenye ziara ya wiki moja,nilikuja kutowa mchango wango kwa shule la mpira la watoto baada yakukutana na Abega nakuhitaji hasa kumsaidia ili aweze kukamilisha ndoto yake. Nia yangu kubwa nikuisaidia Burundi kwa uwezo ninao hadi mumyaka miwili shule hili liwe na timu itakayoweza kuwakilisha Burundi kwenye mashindano yakimataifa. Burundi inavijana wanakao weza , tatizo wanayokosa ni sapoti . Niko tayari kuwapa shavu kadri na uwezo wangu hadi nitakapo ona wamesonga mbele zaidi."
Apo alizuru kwenye ofisi ya Kiongozi wa Atlhletico (Gisage Léopold )

Ifahamike ya kuwa PETER VAN MEERTEN ni Coach wa vijana wasiozidi umri wa miaka 9 ( MEAOCLASS -Amateur Division ) na nyingine ya watoto wa chini ya miaka miaka 14 ( 1st Division Regional ) . Coach huyo ametokea nchini Holland barani Ulaya alishapata fursa yakuonana na baadhi ya Viongozi nchini kama Gisage Leopold (Kiongozi wa Athletico Olympic) , viongozi wa Kinju wanaosapoti shule hilo ,na msiku zakaribuni wanahitaji kukutana na wengine viongozi kama Mama Lydia NSEKERA.
Wachezaji anao funza nchini Holland Coach Van Marteen.

Kwa upande wa Abega kiongozi mbele ya sheria ya shule hio , ni furaha kubwa kumpokea mtu wa maana na mwenye nia kubwa yakuifanyia kazi ndoto yake mumiaka miwili ijayo ili Burundi iwe na timu itakayo weza kuwa tayari yakuiwakilisha .
Alitembelea ofisi ya Kinju,inayosapoti sana shule hilo.

Abega alizitowa shukran kwa wale wote wanao nia yakusapoti watoto nakuwapa bahati yakuweza kuwakilisha nchi yao ,nakumalizia kusema kuwa milango bado ipo wazi kwa yeyote ule atakuwa na mchango wakuendelesha watoto hao ambao tayari wamefikia kwenye idadi ya 125.
Coach Van Marteen akiwa na kikosi cha wasizidi miaka 17 (Under 17)

 Blog yetu hii inamtakia mafaanikio mema...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire