jeudi 5 septembre 2013

Cap Town : PATRICK ERCKHAM azidi kupeperusha bendera ya Burundi pande za Bondeni...
Kwa jina lake halisi  Nshimirimana Patrick almaarufu kama *Erckham* mzaliwa wa Burundi tarafani Nyakabiga barabara ya 1 namba 17 anaendelea kuipaza juu bendera ya Burundi kusini mwa africa Jijini Cap Town / Bellville .Kijana huyo alijikuta  ameingia kwenye game la mziki pale tu alipokuwa akiziskia kazi za wasanii wanao ondoka na style anayotamba nayo kwa sasa hip hop ragga na Rnb akiondoka na hasa hasa na ngoma ngoma kama zile za mitindo ya bongo flava . Kazi  hio ya mziki anayo iendesha pande za kwa Mandela anashirikiana na Producer 1 ambae anamuamini sana akijulikana kwa jina ( DANHO ) kwenye Studio ijulikanayo kama TD Production . Alituhamisha :" Kwa muda huu niko na pini saba  ( Rudi mpenzi, bado najiuliza, nibembeleze, mpenzi wangu, tunawakilisha, mabisho, super club hii ndio ambayo nimefanya clip ila bado haijatoka ,nilifanya nae kazi  Producer James , baada ya hio ninampango wakuachia singo moja na kundi langu la BEEYENFY." Habari ndio hio...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire