lundi 27 mai 2013

Michezo: Vital'o Fc inaongoza Ligi kuu nchini Burundi ( Vital'o Fc 4-1 Espoir ), Neymar asajaliwa na Barcelona leo hii...

ESPOIR MUTIMBUZI
Mchuano ambao ulikuwa umepangwa kuchezwa siku ya Jumaa-mosi kwenye uwanja wa Mwanamfalme Louis Rwagasore nakuahirishwa kutokana na kugawa mipira ya kucheza kwa upande wa Mikoa mbali mbali ya nchi ya Burundi. Mchuano huo ulichezwa leo na ulizipambanisha Timu za Vital'o fc na Espoir Mutimbuzi kutokea Bujumbura Vijijini . Vital'o Fc ilikuja juu kwenye mchezo huo nakuilaza Espoir kwa ushindi wa bao 4-1,nakujiweka pazuri kwenye msimamo wa Ligi nchini . Kwenye wiki ya 14 , Vital'o Fc inaongoza hatamu na pointi 31 na akiba ya bao 22 .
Equipe
GD Pts
1 VITAL'O 22 31
2 FLAMBEAU DE L'EST 10 29
3 ATHLETICO 13 27
4 ROYAL FC 5 23
5 LLB 7 21
6 INTER STAR 4 20
7 MESSAGER NGOZI 0 18
8 ACADEMIE TCHITE -3 18
9 MUZINGA -2 17
10 PRINCE LOUIS -14 12
11 FLAMENGO -20 7
12 ESPOIR -22 5*Klabu ya Barcelona, imekubali kumsajili mshambuliaji matata kutoka Brazil Neymar kutoka kwa klabu ya Santos.
 
NEYMAR

 Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, anatarajia kukamilisha uasajili huo leo siku ya Jumatatu.Kwa mujibu wa taarifa kutoka Barcelona, vilabu hivyo viwili vimeafikiana kuhusu usajili wa mchezaji huyo.

Barcelona imemtaja mshambuliaji huyo kama mchezaji ambaye ana uwezo wa kuwa bora zaidi duniani.
Katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Neymar, alichapisha ripoti kuthibitisha usajili huo na kuwashukuru mashabiki wa Santos, kwa kumuunga mkono katika kipindi cha miaka tisa iliyopita.
Katika taarifa hiyo iliyoandikwa kwa lugha ya Kireno, Neymar, alisema licha ya kuondoka daima moyo wake utasilia na klabu hiyo.
Awali kulikuwa na fununu kuwa klabu ya Real Madrid, vile vile ilikuwa na nia ya kumsajili mchezaji huyo ambaye mkataba wake na Santos ungemalizika msimu ujao.
Neymar atachecheza mechi yake ya mwisho siku ya Jumapili dhidi ya Flamengo, kabla ya kujiunga na Bercelona baada ya fainali za kombe la Shirikisho, ambayo itachezwa kuanzia tarehe kumi na tano hadi thelathini mwezi ujao nchini Brazil.

Katika habari zingine, mshambuliaji matata wa Manchester City Sergio Aquero, amesaini mkataba mpya ambao utaongeza muda wake kwa mwaka mmoja zaidi.
Mchezaji huyo kutoka Argentina ambaye alisaini mkataba wa miaka mitano mwaka wa 2011, kutoka kwa klabu ya Atletico Madrid sasa atasalia na Manchester City hadi mwaka wa 2017.
Aguero ndiye aliyefunga bao lililoifanya Manchester City kunyakuwa kombe la ligi kuu mwaka uliopita wakati walipokuwa wakichuana na QPR.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire