mercredi 6 février 2013

USA: -Aline VYUKA apeperusha vyema bendera ya Burundi USA


Msanii Mrundi wa mitindo ya Gospel na Muigizaji wa filamu anae ishi Marekani DUKUNDE VYUKUSENGE ALINE a.k.a Aline Vyuka ambae alianza kuimba kwenye Chorale akiwa na umri wa miaka 7,na ifikapo mwaka 2012 akawa ameanza kuimba akiwa pekee yake (Single) . Mwaka uliopita mwezi wa July aliweka hewani album yake 'Vyukusenge Vol 1' na baada ya hapo mwezi December aliweka hazarani album yake ya pili 'Dukunde Vol2' na kinyume na hizo mbili ambazo zinatamba sana maeneo ya pande zile anajiusisha na mpango mzima wakuigiza filamu.
ALINE VYUKA anaigiza filamu ila sana sana maandishi matatu (USA) walikuwa wanamfahamu kama muimbaji wa injili yaani anaimba kwakutukuza jina la Bwana YESU katika mitindo ya gospel. Mwaka 2010 filamu yake 'Family issues' iliwekwa hewani na ikajikusanyia sifa kemu kemu kwa upande wawapenzi wa filamu. Mwaka huu wa 2013 ali iweka hazarani filamu yake ya pili 'ORPHANS'. Alitufahamisha ya kuwa yuko na kundi linalo igiza filamu na yey ndio kiongozi wahilo kundi,linajulikana ka 'BAHOWOOD' akitambulika ka Director na Muandishi (Story writer) kwenye filamu zote ambazo zilishatoka. Alimalizia nakutufahamisha kuwa :" Niko naanda filamu itakayojulikana kama INTERPRET,na akipenda mungu mwaka huu lazima niteremke kuja kutembea nchini Burundi... "
Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire