dimanche 2 juin 2013

CONFEDERATION CUP : LLB 0-1 STADE MALIEN...



Jumaa-pili ya leo tarehe 2/June kwenye uwanja wa Mwanamfalme Louis Rwagasore ndipo umechezwa mchuano wa duru ya marudiano kwa upande wa kombe la Shirikisho mchuano wa mchujo wakuawania tiketi yakuingia kwenye makundi ya kombe hilo. Mchuano huo ulishangiliwa na mashabiki wasio kuwa wengi sana,ila walioshabikia Stade Malien walikuwa wengi mno kwani kama mnavyojuwa tarafani bwiza wamejaa,walikuja kushangilia nakupigia fujo waliokuwa uwanjani wanacheza kushinda hata washabiki wa LLB. Bao pekee lilipatikana kupitia mshambuliaji namba 13 wa Stade malien LAMIN DIAWARA . Kwa upande wa Lydia Ludic wachezaji 3 vigogo wakiwemo Idi Saidi Djuma , Ndikumana Yussuf 'Lule' (Nahodha) na Rugonumugabo Stephane hawakucheza kwenye mchuano wa leo kutokana na kadi walizozipata kwenye michezo ya kabla .

Baadhi ya picha :


                                             Matokeo kamili ya mihuano hio ya mchujo : 




Lydia LB Académic (Bdi) 0-1 (0-5) Stade Malien (Mli) *
                                    CS Sfaxien (Tun) 0-0 (0-1) Enugu Rangers (Nga)*
                                    FAR Rabat (Mar) 3-3 (0-1) FUS Rabat (Mar)*
                                    Ismaïly (Egy) 1-0 (0-3)CA Bizerte (Tun)*

                                    Us Bitam (Gab) 2-0 (3-5p) (0-2) Entente Sétif (Alg) *
                                    *Etoile du Sahel (Tun) 2-1 (2-2) JSM Béjaïa (Alg)
                                     ENPPI (Egy) 3-1 (0-2)  St George (Eth)*
                                     Liga Muçulmana (Moz) 2-1 (0-4) TP Mazembe (Cod) *

Kwa upande wa Primus League,siku ya Jumaa-mosi ligi ilikuwa imeingia kwenye wiki yake ya 15 , timu za Mikoani ndizo zilizocheza kutokana na kuwa michezo ilipangwa Jumaa-mosi na kwenye viwanja vyao , ifahamike ya kuwa michuano hio itaendelea katikati na mwishoni mwa wiki hii . Matokeo yalikuwa ifwatavyo :

-Gatumba : Espoir 0-2 Royal Fc.
-Ruyigi : Flambeau de l'Est 3-0 Muzinga.
- Ngozi : Messager Fc 2-2 Inter Star.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire