mercredi 24 avril 2013

CECAFA KAGAME CUP : Vital'o Fc kutetea taji Darfur mwezi July...



Michuano hii itaanza baada ya timu za taifa kuitimisha michuano yakusaka tiketi yakucheza kombe la dunia Bresil 2013 kama alivyoeleza ROGERS MULINDWA kupitia mtnfootball.com.
Cecafa Kagame Cup inazipambanisha nchi 12 za africa ya mashariki na kati ,na nchi hizo ikiwa ni pamoja na : Zanzibar, Tanzania, Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Ethiopia, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan na Sudan yakusini .
Ethiopia ndio nchi itakayopokea michuano hio ,na wao waombwa kuonyesha kuwa wamejianda vyakutosha na wako tayari kuyapokea mashindano hayo hadi mwisho wa mwezi huu. Na endapo hawatokuwa tayari moja kwa moja mashindano hayo yataamishwa nchi nyingine. kama alivyosema NICHOLAS Musonye.

" Walinifahamisha kuwa wako wanatafuta watakao wasaidi (sponsor) ,ni vyema watufahamishe mapema kama itawaweya ngumu ,tutupie macho kwa nchi nyingine ."

Ethiopia ilikuwa inahitaji kupokea mashindano hayo mwezi wa tisa ila Chama cha CECAFA kikasema kuwa ni mbali na vyema ingelikuwa mwezi wa sita (june). Habari kamili kutoka kwenye tovuti ya mtnfootball zimeshaweka hadharani kuwa michuano hio itachezwa nchini Sudan kwenye Miji ya DARFUR  na KORDOFAN. Raisi KAGAME wa Rwanda ndie anaetowa kitita kinachogawanya na timu 3 zinazoshinda toka mwaka 2002 . Bingwa tetezi wa michuano hio ni Yanga iliofunga Mjini Dar Es Salaam bao 1-0 Simba mwaka jana . Vital'o fc ndio itawakilisha Burundi mwaka huu baada ya Atletico Olympic kutofuwa dafu mwaka jana nchini Tanzania.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire