mardi 5 février 2013

Kampuni ya 'IKOH' kwa ushirikiano na Amicales des Musiciens inakuleteyeni "BIRABABAJE" nyimbo ya pole iliokusanya Wasanii 20 kwa niaba yawaliopoteza sokoni...


Kampuni ya Ikoh Multiservice kwa ushirikiano na Baraza la Wanamuziki nchini Burundi (Amical des Musiciens du Burundi), wanajiunga na jamii ya warundi waliopoteza Mali zao katika mkasa wa kuungua kwa soko kuu la Bujumbura ambalo lilikuwa tegemeo kubwa kwa idadi iso isabilika ya wananchii wa Bujumbura,vitongoji vyake hatimae Burundi nzima kwa ujumla. Katika kutuma salam za rambirambi kwa ndugu jamaa na marafiki kwa waliokumbwa na janga hilo, Kampuni ya IKHO imejijumuisha na wasanii wa Muziki nchini Burundi katika kufikisha ujumbe wa pole kwa kutowa wimbo “Birababaje” ikimaanisha “inauma sana,ni uchungu usio kuwa na mfano..”


Orodha ya wasanii walioshiriki kwa kutowa ujumbe kwa wananchi walioathirika na warundi kwa jumla ni hii:Chorus : Rally Joe, John, Florence & Olga

Verse 1 : Rally Joe, John, Shazi kool, Steven Sogo,
Verse 2 : Serge Nkurunziza, Gitero Lax, Alan (Djafris Boyz), Alpha (Divine Glory)
Verse 3 : Chanella, Silas Damara, Lolilo, R Flow, Albert Nkulu, Black G, Mkombozi, Yvan
Bridge : Fabrice (Divine Glory), Patient.


Ikoh Multiservice na Amical de Musiciens du Burundi, inatowa pongezi za dhati kwa wasanii wote walioshiriki katika kufaanikisha kutowa ujumbe huu wa pole kwa waathirika. Habari za ndani tulizozipata toka kwa kampuni hio tulio itembelea jana ni kuwa wako mbioni kuchukuwa picha (Clip video) ya nyimbo hio,ila hadi mdaa huu wangali wanapanga mpangilio mzima wakuitumika kwani zinahitajika picha halisi za tukio na lakufahamu zaidi ni kuwa wanampango wakuzichukuwa picha hizo mahali pale pele sokoni wote wakivalia nguo za juu nyeusi,ishara ya kuonyesha uchungu walio upata kwaku unguwa kwa soko. Nyimbo hio inachukuwa dakika 8 na sekunde ndogo,Alitwambia  BOTCHUM ...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire