jeudi 25 avril 2013

BIG FIZZO atajielekeza South Africa Jumaa-tano hii ( Mercredi,1/May/2013 ) .


Msanii mwenye hadhi na mwenye ujuzi wa hali ya juu kutoka nchini Burundi imepangiliwa  Jumaa-tano tarehe 1/May/2013 ndipo atasafiri kuelekea pande za bondeni kwa mujibu wa habari tulio ipata toka kwake ALLY Q ambae alijihusisha na mpango mzima wamsafara wake . ALLY ni raia kutoka Burundi , na mdogo wake na Referee  wa zamani maarufu sana nchini HICUBURUNDI Jean-Maie Vianney . Alitwambia kupitia mahojiano tuliofanya nae kupitia sim (+2776349914)  kuwa :" Nilipenda kujulisha wapenzi wa MUGANI Desire a.k.a Farious kuwa tumemalizana nae , na akipenda Mungu siku ya Jumaa-tano kinyume na siku ya Jumaa-mosi kama tulivyokuwa tumetangaza mwanzo , palitokea tatizo la makaratasi flani aliopashwa kusafiri nayo ili aruhusiwe kupita uwanja wa ndege . Akipenda Mungu kesho atakuwa tayari amewasili South africa ." Aliongeza nakulonga nasi kuwa :" Tumepanga kuwa atafanya tamasha 2 kwenye Mji wa DURBAN ifikapo tarhe 4/May/2013 , na tarehe 11/MAY/2013 Mjini JOHANESBOURG, ila bado tunafkiria kwa hii kwani tarehe 12 yupo na Tamasha ingine Burundi , ila nina imani atakapo rudi tutamaliza yote kwa maongezi , tumepanga vile vile arushe vumbi Jijini Cap Town ambapo wamekusanyika wakimbizi wengi kutokea burundi  ." Fizzo atakapo toka Bondeni atarejea Burundi atakuwa kwenye Tamasha yake ya mwisho . Kama ilivyokuwa kawaida yetu huwa tunajifunza gisi gani kukufishieni kwa hali na mali habari ambazo zinakuwa zimefanyiwa uchunguzi wa kina , na ndio maana tulichukuwa jukumu lakukuwekeyeni namba hio ya sim kwa ushahidi tosha . Tunamtakia safari njema...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire