mercredi 13 mars 2013

GAGA BLUE :" Mkee wa mtu sio sumu..."

HAKIZIMANA GAEL a.k.a Gaga Blue ni Msanii wa kizazi kipia anaondoka mara kwa mara na mitindo ya hip hop yuko jikoni anarekebisha mambo Maibobo Records baada ya kimia kifupi alichokuwa nacho kwa upande wa production ya nyimbo mpia . Aliongea na safu yetu hii na akawa ametubainishia kuwa :" Dume linapo kaa kimia kila siku huwa linapanga litoke vipi? Mimi kama mwanaharakati wa hip hop nimeamua  kutowa  muono wangu na kuchangia fikra na nyinyi washabiki wangu kutokana na nyimbo *Mkee wa mtu ni sumu * ya kundi QUESTION G walio mshirikisha LOLILO . Nimeika chini nikaumiza kichwa nikaona acha nitafute Msanii wa kike tushirikiane nae,nikawa ni memuomba QUEEN FLO , fikra zangu na zake bikawa bimeingiliana tukaona iko poa na ndio tukawa tumeisimamisha kwa jina la * Mkee wa mtu sio sumu * . Hivi karibuni itawafikieni..." Aliongeza nakutufahamisha kuwa :" Kuna pini nyingine nilio mshirikisha Big Fizzo yenyewe sijaipa jina ila itakufikieni Washabiki wangu very soon..."

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire