lundi 25 novembre 2013

LEAGUE YA TAIFA ITAANZA RASMI tarehe 21/December/2013...

Photo de couverture

Mkutano wakiufundi wa Jopo jipya la kamati tendaji ya Shirikisho la mpira nchini Burundi ulifanyika Jumaa-mosi chini ya usimamizi wa kiongozi mkuu Révérien NDIKURIYO akiwa na wanakamati wenza na Viongozi wa klabu za daraja la kwanza. Pendekezo la Kiongozi mkuu ilikuwa ni Ligi  kuanza kwa ligi msimo wa 2013-2014 tarehe 14/12/2013 ila Viongozi waliomba isogezwe mbele kidogo na ikawa imeamulika kuanza rasmi tarehe 21/12/2013 . Kinyume na miaka ya nyuma , mwaka huu zitajumuishwa timu 14 yaani pataongezeka timu 2 (Guêpiers du Lac na Volontaires kanyosha) ,timu ya Flamengo na espoir zilizokuwa zimetangazwa kuwa zimeshuka daraja zimeachwa , Kiongozi amesema kwenye mkutano huu kuwa kwenye mfumo wao mpya wakuboresha mpira wa miguu nchini wanamulika miaka yakujaa kuzipandisha timu hadi kufkiya Klabu 16 ,na Ligi itakuwa ikichezwa na kati kati mu wiki ili kuwa sambamba na kalenda ya FIFA. Kila kiongozi aliekuwa hapo alipewa nafasi yakuchaguwa karatasi ili atambuwe timu watakayokutana nayo wiki ya kwanza (Tirage au sort) ,Wiki ya kwanza timu zitakutana  ifwatavyo :

* Vital‘O FC vs Guêpiers du Lac
* Prince Louis vs Athletico Olympique
* Académie Tchite vs Flambeau de l’Est
* LLB – Académique vs Muzinga FC
* Inter Star vs Royal FC
* Messager Ngozi vs Flamengo FC
* Volontaires FC vs Espoir FC

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire