mardi 26 février 2013

Docter Jay :" One city one Family bado tupo ."

Msanii wa mitindo yakufoka foka anaezoeleka sana nchini Burundi kama Docter Jay,ambae jina lake lilitambulika sana kwa mtindo wake wakuimba kwakufoka (hip hop) uku akiacha mashabiki kwenye mchaka mchaka na ujumbe tofauti tofauti anao utowa kupitia nyimbo zake binafsi na kwa ushirikiano na kundi lake ambalo wengi wanahisi kuwa limeshasambaratika,nalo silingine likiwa ni 'ONE CITY ONE FAMILY' , aliongea na safu yetu hii nakuweza kubainisha kuwa : " Watu wengi walieikiri 'one city,one family' kuwa imesha sambuka la hasha! Kuna mizunguko zunguko tulikuwa tunafanya kimaisha , kikazikazi tofauti na zaidi sana kazi ya mziki kuna wamoja wame endelea Marekani kama Balozi nawengine kusambaratika Mitoni kama Divin , Zep kay , Mr ganja bila kumtenga Big Dugala na apa Burundi nikiwa nimesalia mimi Dr Jay , Neij na Soso ambae yeye kwa mara nyingi anajishughulisha na karaok siku za nyuma. Kwa ushirikiano nao tumesha jaliwa kurikodi nyimbo tofauti tofauti kama 'mziki na wana mziki' ''Birahagije' 'Turura' 'Nataka money' . Kwa mdaa huu tuko jikoni kwenye Golden star records tunarekebisha pini 'INOTI RMX' kwa ushirikiano na Mshindi wa primusic 2012 NIYINZI Rally-Joe , itakapo malizika itabidi tuchukuwe picha (clip video) za nyimbo hio ili tujitangaze zaidi , na mzizi wa fitna kwa mashabiki ukatwe kwani maneno mitaani ni mengi.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire