jeudi 30 janvier 2014

Hiyi ni habari njema kwa upande wa Wasanii wa Burundi...

Pichani : Big Fizzo , happy Famba , Lolilo na Business man.
Hii ni habari njema kwa Wasanii wa Burundi . Miaka nenda rudi kinyume na Show wanazozifanya na zenyewe hazikidhi maitaji yao , ujio wa Baraza la kulinda kazi za Wasanii mbali mbali nchini O.B.D.E.A ,hali haijabadilika bado kwa upande wa Entertainement nchini , kwani kutwa kucha Wasanii wanalalamika nakutoa maoni yao kupitiya vipindi ,mitandao yao yakijamii nakungineko hali bado ni duni ,pengine ujio wa SHOW BIZ EAST AFRICA waweza kuleta picha nyingine yamafaanikio kwa upande wa Wasanii.
Pichani : Happy FAMBA akiwa na Mkomboz.

 Ujio wa kampuni ya SHOW BIZ EAST AFRICA wakitambulika kwa jina la biashara kama SHOW BIZ MOBILE MEDIA inayopatikana uzunguni , pembezuni mwa Embassy ya Ufaransa tayari wamesimama zaidi kikazi . Wameingia nchini Burundi na CREW nzima kuja kuyaleta matumaini kwa upande wa tasnia ya muziki , inakuja kuwapa shavu wasanii nchini waliozitowa ao wanaozitowa hit song . Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Bw JOSIAH UTUPA akifunguka zaidi kupitiya kampeni yake hiyo anasema :" Tumeamuwa kuja kuwekeza zaidi kimziki ili tuje kuinuwa tasnia ya muziki nchini Burundi , vipaji vipo ni vingi na kiukweli Wasanii wa Burundi wanaweza ila tatizo hawajawezeshwa , na ndio maana tumeamuwa kutimba hadi apa kuja kusaidizana nao ili issue nzima yakuizisha rington za nyimbo zao ieleweke ." 
HAPPY FAMBA akila pozi na sim yake...

Aliongeza nakusema :" Hakuna vigezo vyovyote, hakuna kuchagua huu wala yule,yeyote ule atakae kuwa na hitsong tutawasiliana naye nakumuorodhesha kwenye kampeni yetu hii kwani tuko na Watumishi (CREW) yakuenea . Fahamu ya kuwa Kampuni itakuwa ikichukuwa asilimia 60 huku msanii akichukuwa asilimia 40 . 
Pichani : Mkomboz, T Max na M H.Famba.
(40% pour l'artiste et 60% pour la Maison) , vinginevyo ni kuwa wamekuja nchini na vyombo vyao vyakisasa (Electronic machine) vitakavyo raisisha kampeni hiyo . Siku ya mkotano wa kwanza walijumuika Wasanii wazoefu kama FIZZO , LOLILO , HAPPY FAMBA , MKOMBOZ , T MAX na wengineo walipewa fomu na namba ya siri (code) yakutizama pesa zitakazo kuwa ziki ingia kwenye account yao , Burundi beat inakuahidi kufatiliya kwa karibu...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire