mardi 14 janvier 2014

CHAN 2014 : Burundi 0 - 0 Gabon

Kombe la CHAN linaendelea nchini Afrika ya kusini , mchuano wa mwisho wakufunga wiki ya kwanza ya mashindano hayo ulizipambanisha  timu ya Burundi * Intamba Murugamba* walijitupa uwanjani kumenyana na nchi ya Gabon . Kwenye kundi la D mapema mchana Jamuhuri ya Demokrasia ya congo imeilaza Mauritania`kwa bao _0 .Washabiki tofauti ambao ni Wakimbizi kutoka pande mbali mbali za kwa Mandela waliripoti uwanjani kuipigiya mayowe nchi yao ya Burundi. Timu zote zilikuwa zikisomana kipindi cha kwanza,ila ilionekana Gabon ikiwa mbele . Dakika ya 41 ARAKAZA Mc ARTHUR aliokowa mpira akiwa macho kwa macho na DANIEL COUSIN .
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa timu zote ziki hitaji kuona lango la mungine ,kwa upande wa Burundi Coach Naseem Lofty akisaidizana na  Amars & Mutombola Olivier waliyafanya mabadiliko kwaku mpumzisha Lucio nakumuingiza uwanja Moussa Mossi Hadj na Habonimana Célestin akampisha Shasiri NAHIMANA kiungo wa Inter star kwenye dakika ya 63 . Dakika ya 57 Gaël DUHAYINDAVYI alipewa kadi ya manjano kwa rafu aliyomchezeya mchezaji wa Gabon  mchezaji ambae alimpisha Claude NDARUSANZE kwenye dakika ya 92 , hadi kwenye dakika hiyo Gabon ilikuwa ikiongoza  na kadi 4 uku Burundi ikiwa na hiyo moja pekee . Dakika ya 82 Mungu alipita kati kwani mchezaji wa Gabon alikuwa aandike bao  baada ya ARTHUR kutoka hovyo ikiwa ni kwenye mpira wakutengwa . Dakika ya 90 Gabon iliandika bao ila Refa  Msauza wa mchuano huo akasema kuwa mchezaji aliefunga bao alioteya . Dakika 90 zilimalizika kwa kugawa match yakutofungana ya 0 - 0.

Wachezaji 11 walio anza uwanjani kwa upande wa Burundi ni pamoja na :

-Arthur ARAKAZA 1
-Hassan HAKIZIMANA 17
-Rashid Léon 3
-Frédéric NSABIYUMVA13,
-Issa HAKIZIMANAVidic 15,
-NDUKUMANA YUSSUF Lule 14,
- NDUWARUGIRA Christophe  6,
-Gael DUHAYINDAVYI 2,
-Selemani Yamin NDIKUMANA 20 (Capitaine),
-Célestin HABONIMANA 12,
- Abdul Razzak Fiston 7

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire