mardi 31 décembre 2013

Bongo Movies : Hii ndio idadi ya filamu alizoigiza mzee majuto, na kipato anaochopata kwa mwezi.

Hii ndio idadi ya filamu alizoigiza mzee majuto, na kipato anaochopata kwa mwezi.
Mzee Majuto.
Umeshawahi kujiuliza Mzee Majuto anaweza kuwa anaingiza shilingi ngapi kwa kuigiza kwenye movie zake za vichekesho ambazo mpaka sasa ndio zinashika namba 1 kwa mauzo Tanzania?

Akizungumza na mtandao wa millardayo Mzee majuto amesema ‘kwenye movie za kuigiza sasa hivi kama mtu akitaka kunishirikisha ni lazima unilipe milioni nane kutoka milioni 2 au tatu nilizokua nazikusanya mwanzoni, hii bei nimeibadili kuanzia mwezi September 2013, mimi kadri ninavyocheza movie nyingie za kushirikishwa ndio nazidi kujipunguzia kipato changu kwa mwezi kutoka kampuni ya STEPS iliyoniajiri’
‘Mpaka sasa nimecheza movie zaidi ya 600 toka nimeanza kuigiza za kushirikishwa na zangu mwenyewe, nilianza kulipwa zaidi ya milioni moja kwenye movie toka mwaka 2007/2008 baada ya kuwa na kampuni ya Ally Riyami ambae alikua ananilipa shilingi laki sita kwa kila movie ya Comedy kwa hiyo kwa mwezi napata mpaka kwenye milioni 6 au saba kutokana na idadi ya movie nitakazoigiza’ – Mzee Majuto
‘kwa sasa hapa Steps nalipwa kuanzia milioni 17 mpaka 20 kwa mwezi, ni malipo mazuri sana ambayo napata kila mwezi na nimepangiwa kucheza movie 9 kwa mwaka lakini kule Ally Riyami kwa mwezi ndio nilikua nacheza hizo movie 10, yani unacheza movie nyingi mpaka unasikia kizunguzungu…. kwa sababu nilitakiwa kucheza movie 1 kila baada ya siku tatu ila kwa sasa kwenye mkataba wa Steps nacheza movie moja ya kampuni na moja ya nje ya kampuni, maisha mazuri’ – Mzee Majuto
Source : BM

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire