Jana Jumaa mosi tarehe 24/8/2013 kwenye uwanja wa Mwanamfalme Louis
Rwagasore ndipo palipochezeka mchuano wa kwanza kwenye ngazi ya Nusu
fainali. Jana kwenye uwanja huo watani wa jadi wawili Lydia Ludic
burundi academic ilimenyana na Atlhetico Olympic kwakuwania tiketi
yakuicheza fainali ya kwanza ya kombe lilochukuwa na fasi ya kombe la
Raisi miaka 3 ya nyuma na kubatizwa jina la Kombe la Shirikisho ( Coupe
de la Confederation ) . Anakae tunzwa tunzo hilo moja kwa moja anakuwa
balozi wa Burundi kwenye ngazi ya kombe la shirikisho barani africa kama
inavyo iwakilisha Burundi LLB miaka 3 iliopita . Mchuano wa jana
ulikuwa ni wavuta nikuvute kwani timu zote 2 kila moja iliwasili
uwanjani kuja kuonyesha kipi unacho cha ziada kwa nyingine timu .
Wachezaji wa Athletico ka Ciza Hussein na Nahimana Claude almaarufu kama
Papa Claude wanao semekana kuwa watajiunga na Mukura ya Rwanda kwa
ushirikiano na wenzao walionyesha kandanda safi na kosa kosa zikawa
nyingi kwenye lango la LLB lililo lindwa na mkongwe Nyabenda Athanase
alias Tchimba alie onekana kuwa mpole sana na mtulivu golini . Kosa kosa
hizo za Athletico zilikuja kuwasababishia kufungwa bao na NDARUSANZE
Claude baada ya shuti kali iliopigwa kama mshale na NDUWARUGIRA
Christophe alias Lucio ,mpira huo maskini ya mungu Nduwimana Saidi alias
Tamaa ulimshinda ukawa umemtoka na ndipo Claude ali iwezeshea timu yake
kupata bao hilo muhimu sana ilikuwa ni kwenye dakika ya 44 ,dakika 1
kabla ya muda maalumu kumalizika wa kipindi cha kwanza . Walipotoka
mapumzikoni hapakuwepo mabadiliko yeyote ngambo zote mbili kwa mmoja kuona lango la mwenzie. LLB ina sura nzuri yakuchukuwa tunzo hilo baada yakulitetea taifa vyakuridhisha
kwenye michuano hio yakibara miaka 3 ya nyuma na hadi walipofika kwenye
mchuano wa mwisho ungeliweza kutuma wafike hadi kwenye duru ya makundi
mwaka huu baada yakuchapwa kitunga cha mabao na timu tajiri ya Mali
STADE MALIEN (5-0 , 1-0 ) . Matumaini ni yote kwa upande wa Mkufunzi
TUHABONYE Michel ambae anakiri kwa udi na uvumba lazima wanyakuwa tunzo
hilo . Nani watakae pambana kwenye fainali ? Timu itajulikana kwenye
mchuano wa leo kati ya Academie Tchite na As Tanganyika , timu ya daraja
la pili ambayo ilifika mwaka huu kwenye ngazi hio...Wait and see.
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire