'Ahadi ni deni' hio ni mesali yakiswahili inayomaanisha kuwa ni vyema unapo towa ahadi utimize, hio imekuja baada ya Msanii NIYINZI RALLY-Joe kujishindia tunzo ya mashindano yaliokuwa yameandaliwa na kampuni ya Brarudi kupitia kinywaji 'PRIMUS' na ndio maana kuitwa 'Primusic' yaani waliunga kinywaji Primus na Music kwa manufa ya Wasanii wa Burundi nzima . RALLY-JOE ameondoka jioni ya jana saa kumi na mbili na dakika 20 (18h20') na ndege aina ya Kenya Airways. Duru toka kwa Excellent NIMUBONA ambae alikuwa anajishughulisha na mpango mzima wakupasha habari kwenye mashindano hayo alitufahamisha kuwa :" Ameondoka iyo mida (12 na dakika 20 jioni) ameitika wito wa KIDUM NIMBONA JEAN-PIERRE ambae yupo Nairobi anamsubiri , baadae watarikodi nyimbo wakiwa wote kama tulivyotangaza kabla kama mshindi atapata milioni 10 na kupata fursa yakurikodi na Mwanamuziki mwenye heshma zake KIDUM nyimbo ya audio na video." Ifahamike kuwa hatujapata fununu ya nyimbo hio itakavyo itwa na Studio ipi itakayo jishughulisha nakuirikodi . Itaendelea...
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire