vendredi 11 octobre 2013

India : MITUN CHAKRABORTY na AMITABH BACHAN bado wangali wanaigiza japo umri unazidi kurepa....

Amitabh bachan
Akiwa ana umri wa miaka 70 sasa tangu amezaliwa Oktoba 11, 1942, mwigizaji mkongwe wa India, Amitabh Harivansh Bachchan bado anacheza filamu na sasa ameingia anga za Hollywood baada ya umaarufu mkubwa Bollywood aliojipatia kuanzia miaka ya 1970 mwanzoni tu. Mwaka huu, mkongwe huyo ametoa filamu mpya ya Hollywood iitwayo The Great Gatsby akicheza kama Meya Wolfsheim dhidi ya Leonardo Dicaprio na Tobey Maguire. Hii ni filamu yake ya kwanza Hollwood.

Mithun Chakraborty.


Gouranga Chakraborty, maarufu kama Mithun akiwa ana umri wa miaka 63 tangu amezaliwa Julai 16, mwaka 1950 pia bado anaigiza, ingawa yeye ni Bollywood tu. Mithun aliyeibukia katika filamu ya Mrigayaa mwaka 1976, filamu zake za karibuni ni pamoja na Veer (2010) akiwa na Salman Khan, Golmaal 3 (2010) akiwa na Ajay Devgn, Housefull 2 (2012) akiwa na Akshay Kumar, OMG – Oh My God! (2012) akiwa na Akshay Kumar, Khiladi 786 (2012) akiwa na Akshay Kumar na Enemmy ya mwaka huu akiwa mwanawe mwenyewe, Mimoh Chakraborty na Sunil Shetty.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire