dimanche 15 septembre 2013

RONALDO SASA NDIYE MWANASOKA ANAYELIPWA KULIKO WOTE DUNIANI,VITAL'O 1-2 ATLETICO (Nusu fainali ya Super Primus League)

Real deal: Ronaldo says he wants to end his career in Madrid
CR7 na Florentino Perez (Kiongozi wa Real Madrid)


MRENO Cristiano Ronaldo amesaini Mkataba mnono wa miaka mitano kuendelea kuichezea Real Madrid, wenye thamani ya Pauni Milioni 76 (zaidi ya Euro Milioni 90) inayomfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani na amesema anataka kustaafu soka yake Madrid.
Ronaldo amesaini Mkataba huo Santiago Bernabeu leo na rais wa klabu, Florentino Perez siku moja baada ya kufunga Madrid ikitoa sare ya 2-2 na Villarreal.Kiwango hicho kinamfanya awe analipwa karibu mara mbili ya malipo ya Gareth Bale na kinarejesha heshima yake baada ya kupoteza hadhi ya mwanasoka ghali duniani, kufuatia Real kumnunua Bale kwa Pauni Milioni 86.

Ronaldo akizungumza na vyombo vya Habari Hispania baada ya kusaini Mkataba mpya,alizungumza :

"Nawakubali mashabiki wanavyonipenda hapa. Nina furaha, nataka kuonyesha mavitu yangu uwanjani. Nitakuwa mkweli kwako- kila mmoja anajua nilikuwa Manchester kwa miaka sita. Manchester ni ya kale sasa. Sasa klabu yangu ni Real Madrid. Hii ni nyumbani, familia yangu iko hapa na nina furaha haswa hapa.

"Naziheshimu klabu zote zilizonitaka. Lakini wakati wote wanafahamu uamuzi wangu, kwamba lengo langu ni kuwa hapa na kucheza labda, pengine, mwisho wa maisha ya soka."Yajayo hakuna ajuaye.

Leo ndipo timu ya pili ilifahamika kwenye uwanja wa Mwanamfalme Louis Rwagasore kati ya Lydia Ludic Burundi Academic na Vital'o Fc ,mchuano huo ulichezwa na ukawa ni faida kwa Atletico kuitumia na fasi ilio ipata kwakukosekana kwa wachezaji kadhaa wa Vital'o kujikatia tiketi yakuchuana fainali ifikapo tarehe 29/9/2013,siku ambayo zitatolewa tunzo zote za msimo huu wa 2012-2013 . Ifikapo tarehe 22/9/2013 ndipo LLB itachuana na ACADEMIE TCHITE fainali ya kombe la shirikisho.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire