jeudi 5 septembre 2013

KAZE GILBERT na TAMBWE AMISSI wako kwenye hali nzuri Tanzania kwenye timu ya SIMBA SC...

Pichani: Kikosi cha Simba wakiemo Tambwe na Gilbert
Wachezaji wawili kutokea nchini Burundi KAZE GILBERT alias DEMUNGA na TAMBWE AMISSI wanaendelea vyema kwenye timu yao ya SIMBA sports Club waliposajiliwa  mwaka huu kutoka kwenye timu ya Vital'o Fc bingwa tetezi wa kombe la  CECAFA nchini Sudan ya kaskazini . Kwa muujibu wa habari tunazo kutokea pande zile nikuwa wachezaji hao wawili wamekuwa kitegemeo sana kwenye klabu hiyo ya Simba ambayo ilibadili wachezaji wengi nakusajili vijana wenye hari na uzowefu wa hali ya juu . Nilipata fursa yakuhojiana nao kupitia ukurasa wa kijamii wa facebook na wakanieleza haya yafwatayo :

* Demunga :" Niko kwenye hali nzuri ,washabiki jopo nzima la ufundi la timu yangu wananipenda sana na iki nikitu chakujivunia , ntajitaidi kadri niwezavyo niji imarishe vyakutosha na alakuli hali nisalie kwenye 11 wanakao anza uwanjani , bado ingali mapema ila insha'allah nina imani tutafika mbali na timu hii."

* Tambwe : " Nimeakikisha msimo uliopita kukusanya taji zote za mfungaji bora nchini Burundi ( Primus league , Confederation Cup na bila kuhasahau CECAFA ,haina budi kuwa na hapa Simba msimo huu itakuwa sambamba kwani hakuna utofauti mkubwa ninakao uona kwa upande wawachezaji nakao cheza nao hapa, Mungu akipenda ntafanya vizuri zaidi kwani kila siku kunapo nia njia  inakuwa karibu sana."

Ifahamike ya kuwa Simba inaendelea na mazoezi yake jijini na wachezaji wake wote wapo katika hali nzuri na tayari kwa ajili ya mechi hiyo.
Mechi hiyo itaanza majira ya saa 11 jioni ili kuwezesha watu wengi kwenda uwanjani kutazama mechi hiyo ikizingatiwa kuwa Ijumaa ni siku ya kazi.
Wakati huo huo: Kufuatia tangazo la Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage, kuhusu Mkutano wa Katiba uliopangwa kufanyika Novemba mwaka huu, klabu imeanzisha rasmi mchakato wa kuwa na Katiba Mpya itakayokwenda na wakati.

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire