dimanche 28 juillet 2013

Habari za uhamisho kwa upande wawachezaji wa Burundi...


Tambwe asaini Simba kandarasi ya miaka 2.
Kwa Burundi kutambuwa uhamisho wawachezaji ikiwa ndani na nje ya nchi inakuwa sio rahisi , kutokana na uchunguzi wa kina tulio ufanya kwakutafuta habari kwa upande wawachezaji na viongozi tofauti tofauti gisi waweza kuzihama Timu zao tulikukusanyieni baadhi ya wachezaji wanaoweza kuzihama timu zao na wengine tayari wamesha saini kwenye timu tofauti za nje ya nchi. siku baada ya siku endapo habari mpya itakuwa inapatikana tutakuwa tukiwafikishieni :
Fuadi anasaini kandarasi ya miaka 2 kwenye timu ya rayon Sport.

Vital'o Fc
-----------
* Kanyekore Gilbert Kagabo Yaounde : Tayari kishajiunga na klabu ya Kiyovu sport ya daraja la kwanza nchini pale ilioshika na fasi ya 8 kati ya timu 14 zilizopambana kwenye msimo wa Primus league 2012-2013 , inasemekana kuwa anaweza kwenda Rwanda pamoja na Wachezaji wawili ndugu Girukwishaka Michel na Girukwishaka John.

* Tambwe Amissi : Tayari kisha saini kandarasi ya miaka 2 na Simba ya Tanzania,ila kuna timu ya Saudia Arabia inamsaka kwa udi na uvumba ili aweze kujiunga nayo.

* Kaze Gilbert Demunga : Habari tulizo zipata nikuwa nayeye atasalia kwenye timu hiyo,inasemekana atakapo tuwa Burundi baada ya mchezo wa leo na Sudan atajielekeza Dar es Salaam kusaini kwenye klabu ya Simba. Ila apo awali alikuwa ametajwa kujiunga na klabu moja wapo kutokea nchini South africa.

Ndikumana Yussuf Lule : Mchezaji kiungo na roho ya timu hiyo alio utowa mchango mkubwa nakuiwezesha timu yake kufanya vyema kwenye mashindano tofauti anatafutwa na Rayon Sport. Habari ya mwisho tulio ipata kwa upande wa mchezaji huo ni kuwa mwanzo wa wiki hii kuna tume ya viongozi wa timu ya Rayon Sport watakao wasili Bujumbura kwa mazungumzo na viongozi wa Vital'o.

Saidi selemani : Anauliziwa nchini Dubai,inasemekana kuwa mambo ya soa aliweka kando na kwasasa anajihusisha kutafuta pesa kwakutumia njia nyingine kinyume na mpira.

* Nzigamasabo Steve : Yeye ameazimwa miezi 6 kwenye klabu ya Enugou rangers,duru kutoka pande zile zinasema kuwa tayari ameshazoweya hali ya hewa na kuna baadhi ya michuano alishacheza. Ifahamike ya kuwa mwaka jana alitaka kujiunga na Klabu ya Saint george ya Ethiopia ila baadae timu mbili hazikukubaliana na akwa amerejea Burundi , ila mwaka huu kijana huyo amebahatikiwa na yupo Nigeria kwenye timu ya Enugou Rangers.( Pret contrant ya miezi 6).

* Nani Coach atakae mrudilia Kanyenkore? : Wanao zungumzwa kuwasili na kujiunga na timu hio ni pamoja na : Coach Okoko ambae alikuwa mchezaji wa zamani wa timu hio. Fununu zingine zinasema Coach Olivier Mutombola,coach wasasa wa Flambeau de l'Est ya Ruyigi nayeye vile vile aliwahi kuwika kwenye timu hiyo ya Vital'o. Anazungumzwa vile vile Coach Mupenda Mohsin ambae kwasasa hana timu yeyote licha ya vijana anao nowa wa daraja la 4 (Mukukwe).
Papy Faty

Atlhetico Olympic
---------------------
* Ciza Hussein na Nahimana papa Claude wao inasemekana kuwa waweza kujiunga na klabu ya Mukura Victory Club,kupitia jarida la Ruhagoyacu,jarida la Mjini Kigali liliwahi kuchapa habari hio nakusema kuwa Coach mkuu wa timu hio Kaze Cédric alipendekeza wachezaji 3 kutokea Burundi (Papa Claude,Ciza na Lucio)  kuweza kujiunga na klabu hiyo anayo inowa,ikumbukwe ya kuwa Mukura ilisimama kwenye na fasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi msimo uliomalizika.
Saidi Ntibazonkiza

Lydia Ludic Burundi Academic
-----------------------------------
Hakizimana Issa Vidic anaweza kuhama klabu hio ila wapi atahamia? Tunachunguza habari yenyewe kwani alipo ongea na safu yetu hii alitubainishia kuwa anasubiri kauli ya mwisho kutoka kwa Lionnel (Président d'honneur wa Lydia ludic Bdi academic ) .

* Nduwarugira Christophe Lucio anaweza kujiunga na timu ya Mukura Victory ya Rwanda ila bado wangali kwenye mazungumzo.

Rugonumugabo Stéphane alias  Rugo anatafutwa na Azam ya Tanzania , ila hakuna ujumbe wowote timu yake yasasa ilishapata kutokea Dar es Salaam.

* Type Bolima Matembe inasemekana kuwa yuko kwenye mazungumzo na timu ya Daring Club Motema Pembe kutokea Mjini Kinshasa.Ifahamike ya kuwa ni mchezaji mwenye asili ya Goma kwenye klabu ya Virunga.Ila timu yake ya kwanza alio ichezea Burundi ni timu ya Vital'o Fc.

* Duhayindavyi Gael, Ndarusanze Claude  wanadai kuongeza kandarasi yao kwakuzidi kuichezea klabu hio ambayo inamuelekeo mzuri wakunyakuwa taji mbili msimo huu.

Royal fc
----------

* Ishimwe Muhidini Issa alias Zappy yuko kwenye mazungumzo na klabu ya Unité ya Muyinga,duru tulio ipata kutoka kwa viongozi wa klabu ya Unite zinasema kuwa mazungumzo yamefikia ukingoni na hatma ya kandarasi yake ya miaka 2 yaweza kufikia hadi milioni 6 sarafu za Burundi.

* Sinzinkayo Fabrice (nahodha wa timu hiyo) anasakwa na klabu ya Vital'o Fc,baada yakuichezea timu ya Athletico olympic mwaka 2010,kijana huyo anasema kuwa amechoka anahitaji kubadili mazingira .

* Nduwimana Jean Gentil anasakwa na klabu ya Vital'o Fc kuja kuliziba pengu la Tambwe Amissi ambae tayari kisha saini mkataba wa miaka 2 na Simba ya Tanzania .
                                                              
# ( Nje ya Burundi )
                                                            
Rwanda :
* Rayon Sport :
-Imewaongezea kandarasi ya miaka 2 wachezaji wawili wa Burundi waliowahi kuwiki miaka ya nyuma na hadi mdaa huu nchini pale Fuadi Ndayisenga na Nizigiyimana Karim Makenze. Walisaini dakika za mwisho huku hatma yao ilikuwa inasemekana kuwa Kiyovu Sport ilikuwa tayari kuweza kuwasajili.

- Amissi Cedric,mchezaji machachari,mwenye ujuzi wa hali ya juu inasemekana kuwa anaweza kujiunga na klabu ya AC LEOPARDS ya kenya , ni klabu anayo ichezea Tambwe Floribert .
- Fiston Abdurazzak amesaini kandarasi ya miaka miwili kwenye timu hio.

* Kiyovu sport
- Yaweza kuwasainisha wachezaji wawili kutoka kwenye klabu ya Vital'o Fc Girukwishaka John na Michel ,habari hii bado inafanyiwa uchunguzi wa kina...


* Wachazaji hawa watasalia kwenye timu zao :

- Yameen Selemani Ndikumana  atasalia kwenye timu ya El mereikh-Sudan

- Ntibazonkiza Saidi  atasalia  Cracovia Craco- Poland,ila ilikuwa inasemekana kuwa anaweza kwenda spania mwaka huu.

- Papy Faty atasalia kwenye timu yake ya Bidvest,ila kuna habari zinasema kuwa yuko anatafutwa kwa udi na uvumba na klabu ya Kaiser Chiefs.Tunafatilia kwa karibu...

- Tambwe Floribert atasalia kwenye timu ya Ac Léopards ya Kenya .

-Kwizera Pierrot atasalia kwenye timu yake ya AFAD , daraja la kwanza nchini Ivory Coast .

-Nzokira Jeff atasalia kwenye klabu yake A S A S Djibouti Telecom,ila kuna habari zinasema kuwa anaweza kurudi kujipima tena nchini Yemen kwani mwaka jana alienda walishafunga dirisha la usajili.

-Manirakiza Haruna Lucio na Afizi wao bado wapo kwenye timu ya Lupopo nchini DRC,mjini Kinshasa.

- Mavugo Laudit anaweza kusalia kwenye timu ya AS KIGALI ilioshika nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi msimo uliomalizika.

-Didier Kavumbagu atasalia kwenye timu yake ya yanga bingwa tetezi,aliteuliwa kuwa mchezaji aliependwa zaidi msimo uliopita.

Walitamba Burundi ila amfahamu wapi walipo :

* Belgium :

- Mutambaro Ismael

-Amran alikuwa mshambuliaji wa Inter Star.

-Eric Ndizeye

* Rwanda

-Yussuf Tchami

* Mayotte

- Alfani Rehani

Fahamu vizuri : Kutokana na maombi yenu wapendwa wasomaji wa Blog hii tuwa mengi kuhusikana na habari za Wachezaji warundi ulimwenguni,tuna ahidi kuendelea tunafanya uchunguzi wa kina nakukuleteyeni habari zilizofanyiwa uchunguzi wakina.Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire