jeudi 23 janvier 2014

CHAN 2014 : 125.000$ ndizo pesa Burundi imepata baada yakushika na fasi ya 3 kwenye Kundi D .


Baada yakuondolewa wana na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ( DRC) . Duru za Timu ya taifa ya Burundi tulizozipata mpaka sasa ni kuwa watawasili Bujumbura kesho mchana , vinginevyo ni kuwa usiku wa Tarehe 1/2/2014 , mshindi wa Kombe la tatu la Mashindano ya CHAN , South Africa 2014 , atajikusanyia pesa 750.000$ . Wa pili atajikusanyia 400.000$ .

Idadi ya timu 16 zilizo shiriki kwenye mashindano hayo kila timu itapata pesa kulingana na walipofkia kwenye mashindano hayo . Watashindana ifwatavyo :

- 250.000$ watagawana wa 3 nawa 4 .
- 175.000$ kila Timu itakayo agaa mashindano kwenye duru ya Robo fainali ( 1/4 finale)
- 125.000$ kwa timu ilieshika na fasi ya 3 kwenye duru ya mtoano kwa upande wamakundi .
- 100.000$ kwa timu ilieshika na fasi ya 4 kwenye makundi .

Jumla ya milioni 3,2 $ ndizo zitagawiwa Timu zote 16 . Kumbuka ya kuwa fkra ao idea yakuanzisha Kombe hilo ilikuja mwaka 2007 kupitia Kiongozi wa Shirikisho la Dimba barani Afrika ISSA HAYATOU , kombe hilo la kwanza lilichezwa mwaka 2009 nchini Ivory Coast na mshindi ikawa DRC .

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire