mercredi 26 juin 2013

ALI KIBA na Dr CLAUDE wanasubiri kwa hamu sana nchini...

Matayarisho ya bonge la Tamasha linalo andaliwa nchini kwa kuwakaribisha wasanii nyota toka pande za kanda ya afrika mashariki wakiwemo ALI KIBA (King of Bongo Flava) na NIYAMUREMYE Claude Abdallah a.k.a Docter Claude (Rwanda) ,ifahamike ya kuwa ni mzaliwa wa Burundi ila tayari amekabiziwa na uraia wa Rwanda. Kwa muujibu wa ripoti tulizo zipata kwa niaba ya wanao jihusisha na maandalizi ya Tamasha hio ni kuwa walituwekea wazi kuwa mambo yote yanakwenda vizuri,ratiba ilivyopangwa haijabadilika bado. Mwishoni mwa jumaa ALI KIBA na Dr CLAUDE watakuwa tayari nchini kwa mkutano na waandishi wa habari ili waweke kinaga ubaga ujio wao na  zawadi wanayokuja nayo kwa jamii ya Burundi . Blog yenu hii imekwenda mbali zaidi nakuitaji kujuwa kipi wanachofkiria raia wa Burundi kuhusikana na ujio huo baada ya DIAMOND PLATUNMZ aliporusha vumbi mapema miezi iliopita. Baadhi ya raia walitwambia ifwatavyo :

* Julia : Mimi nampenda sana Ali Kiba kwani anaimba vizuri na nitafurahi nitakapo pata fursa yakupiga nae picha....

* Karim : Ali Kiba ndie King wa Bongo flava,namkubali lazima tumsapoti...

* Bizimana : (Jewe mba i Gitega ,ningombwa ko manuka i Bujumbura kumuraba,nsanzwe nkunda na Dr Claude ) Mimi naishi Gitega ila lazima niteremke Bujumbura kumpa sapoti ,nampenda tena Dr Claude...

* Florent : Mimi naisha Uvira, Cocktail Beach nikaribu naomba wapenzi wa Ali Kiba tujumuike Burundi kumpa sapoti...

* Goreth : (Nzoba ngiye gushigikira abasani babarundi mugabo nabo batumire tuzoba turikumwe , akimaanisha : Ntakuwa nimekwenda kuwapa shavu wasanii wa Burundi ila hata wageni lazima niwapigie mayowe.
Ifahamike tu ya kuwa Wasanii wote wanaopatikana kwenye bango hio wa hapa nchini wanajianda kutwa kucha ili kuweza kuwaridhisha washabiki wa buja flava na wapenzi wa mziki kwa ujumla.
Business man / Famba

Business man alitwambia kuwa :" Lazima niwakualishe wageni , ntawaonyesha kuwa mimi ni mkali wa show..."

1 commentaire: