dimanche 3 mars 2013

Kigali : -Kundi la Buyenzi la wapiga ngoma *RUCITEME KARYENDA* wametunzwa na walio anda FESPAD mwaka huu...

Jana Jumaa-mosi ndipo maonyesho na mashindano ya FESPAD nchini Rwanda yaligonga ukuta uku nchi zilizoshiriki kuonyesha ubabe nakutunzwa kwakazi walio ifanya yakuridhisha .kama kawaida nchi yetu ya Burundi inapo kwenda kwenye mashindano hairudi mikono mitupu, Burundi kupitia kundi la Wapiga ngoma RUCITEME KARYENDA la mtaani Buyenzi limejinyakulia tunzo ambalo ni muhimu sana kwa nchi yetu ya Burundi. Kwa upande mungine ni kuwa wageni wote waliokuwa kwenye orodha nikizungumzia nchi zilizokuwa zimealikwa zote ziliwasili na Tamasha ilikuwa babu kubwa kabisa . Kidum aliwakubalisha kwa mara nyingine tena wapenzi wa mziki walibaki na deni kwani pande zile live music hazipigwi kimataifa kama wanavyofanya warundi. Walio itika walikuwa wengi,pembe kama zote za AMAHORO STADIUM zilifurika. Mashindano hayo yamulikiwa kufanyika baada ya miaka miwili . Habari ndio hio...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire