jeudi 27 juin 2013

Top 10: Ndani ya mwaka mmoja wametengeneza mamilioni ya Dola, Wanapendwa zaidi na watu duniani, Na hawa ndio ma-celeb wenye nguvu na ushawishi zaidi duniani


 Katika orodha hii nafasi ya kwanza kabisa anashikilia mwanamama Oprah, na hii ni kutokana na nguvu yake kubwa katika Televisheni pamoja na mitandao ya kijamii, na pia anamiliki wa Cable Network kubwa kabisa ya Oprah, na kwenye rekodi inaonyesha kuwa kati ya mwezi June 2012 na June 2013 amejivunia kiasi cha dola milioni 77.
Katika nafasi ya pili anasimama, Lady Gaga ambaye ana nyota ya kupendwa na watu kutoka kona zote za dunia, akiwa anaongoza kufuatwa katika social networks hasa kutokana na muonekano wake wa kitofauti zaidi na Uwezo kimuziki, licha ya kuwa nnje ya stage kwa muda akiwa anapona uparesheni ya hips, ameweza kujivunia dola milioni 80 katika kipindi cha mwaka jana mpaka mwaka huu.
Katika nafasi ya tatu anasimama TV/Film Director/Producer maarufu Steven Spielberg ambaye yupo nafasi ya juu kabisa na anaheshimika katika fani hiyo akiwa ni mtu mzima mwenye umri wa miaka 59, Huyu kwa mwaka amejitengenezea dola milioni 100.
Katika nafasi inayofuata anasiamama mwanadada Beyonce ambaye mafanikio yake yanafahamika kote, akiwa amejivunia dola milioni 53.Pia kuna mkongwe Madonna katika nafasi ya tano, akiwa ametengeneza dola milioni 125.

Nafasi ya sina inashikiliwa na Taylor Swift, dola milioni 55.
Nafasi inayofuata inakamatwa na Jon Bon Jovi, dola 79.
Nafasi ya saba inashikiliwa na mwanamichezo wa Tennis, Roger Federer ambaye anashikilia dili nono na makampuni makubwa mbalimbali hasa yale yanayofanya biashara ya vifaa vya michezo, dola milioni 71.

Nafasi inayofuata inashikiliwa na mwanamuziki kinda, Justin Bieber, dola milioni 85.Na katika nafasi ya 10 yupo mtangazaji mkali kabisa wa TV, Ellen DeGeneres, huyu akiwa na dola milioni 83 ndani ya mwaka mmoja.
# Vigezo vya Forbes katika orodha hii vimezingatia mapato waliyoingiza wasanii hawa kutoka mwezi Juni mwaka jana mpaka mwaka huu, na pia namba ya watu ambao wanawatazama na kuwafuatilia kwa karibu.


Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire