jeudi 23 mai 2013

Dar Es Salaam : Didier KAVUMBAGU avutia wapenzi wengi wa Soka baada ya msimo kumalizika nchini Tanzania...



Baada ya pazia la Ligi Kuu Tanzania bara kufungwa rasmi jumamosi iliyopita na Yanga kutwaa ubingwa, huyo ndiye mchezaji aliyenivutia zaidi kwenye ligi hiyo… Anaitwa Didier Kavumbagu, ni mchezaji wa kimataifa kutoka Burundi.

Binafsi namkubali huyu mshkaji pia mashabiki wote wa Yanga tunamkubali… Ni mchezaji mwenye uwezo wa kuubadilisha mchezo kwa muda wowote na goli nyingi alizofunga msimu uliopita, alikuwa akitumia akili sana!
Baada ya Ligi kuu kumalizika, Didier Kavumbagu amejijengea sifa kubwa hapa nchini…
Mfano ni hilo banda nimekutana nalo katika mizunguko yangu ya siku zote, nimekutana na banda hilo maeneo ya Mwenge, jijini hapa Dar es Salaam. Mmiliki wa banda hilo, ambaye anauza mabegi na viatu vya mtumba, ameniambia yakuwa kwenye klabu ya Yanga, anamuona Didier kama mchezaji namba moja mwenye ujuzi mkubwa… Na hiyo ndio sababu kaamua kuandika jina la mchezaji huyo hapo kwenye banda lake…
Pia maeneo ya Mbagala kuna saluni yenye jina lake Didier Kavumbagu na majuzi kati nimekutana na daladala maeneo ya Buguruni lenye jina hilo la ''Didier Kavumbagu''…
Hiyo sio sifa kwa Didier peke yake, bali ni sifa kwa taifa nzima la Burundi…
You deserve, Didier!… Mashabiki wote wa Yanga, we are proud of you, my bro!…
Tunakutakia kila la kheri msimu ujao…

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire