lundi 1 avril 2013

BOTCHOUM PRO, PRODUCER ASIE CHAKAAUtakuwa ni ukosefu wa fadhila iwapo utauzungumzia muziki wa kizazi kipya nchini Burundi bila kutaja jina la Producer Botchoum Pro, aliejizolea sifa tele katika kuandaa na kutengeneza muzizi wa wasanii wengi wa kizazi kipya walioibuka miaka ya 90 na kuanza kuonyesha makeke kwenye tasnia hii ya Muziki ambayo ilianza kitambo tu, na Wasanii waliobeba majina makubwa kama vile akina hayati Chanjo Amisi, Christophe Matata, Afrika Nova Bahaga Prosper na wengine ambao waliwavutia sana wapenzi wa muziki wa Burundi katika zama hizo.


Kwa jina halisi ni Kwizera Freddy Khaled maharufu kama Botchoum alianza kucheza muziki kama Disc Joker ama DJ na baadae kuwa muandalizi wa Muziki kwenye Studio ya kwanza aliko anzia Felix Music iliokuwa chini ya mkono wa Felix Music aliekuwa DJ katika Club Archipel mwaka 2003.

Akiwa Feliz Music aliweza kutengeneza nyimbo za wasanii wengi chipukizi walioibukia tasnia ya muziki wa kizazi ambao leo wamejijengea majina na wengine waliaomuwa kuondoka kwenye game la muziki.


Akilonga na Ikoh Biz Botchum amesema kwamba katika kipindi hiki tayari amepata mafaanikio makubwa lakini pia amekuwa akikutana na misukosuko ambayo ni kawaida katika kila nyanja ya maisha kukumbana na mauzauza.

Botchoum amesema kwamba ndoto yake kubwa ni kujiimarisha zaidi katika kazi yake, ili siku moja aweze kufanya kazi na wasanii wakubwa Dunia.

Kwa sasa Botchoum amesema anatulia kwenye Studio ya Kampuni ya Ikoh Multiservice kuhakikisha anainuwa wasanii wengi ambao wanania ya dhati ya kusonga mbele kwenye kwenye tasnia hii ya Muziki ambayo amesema inahitaji bidii ya kutosha na nguvu za ziada ili kuendelea kuwepo kwenye muziki.

Source : Ikoh

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire