dimanche 10 mars 2013

Primus League : Royal 1 - 0 Flamengo (Msimamo kamili wa duru ya Awali)...

Ligi ya taifa maarufu Primus league Jumaa-pili ya leo ndio imegonga ukuta,pambano ya mwisho ilizipambanisha timu ya Flamengo ambayo nyumbani ili ipokea Royal kutokea Muramvya . Pambano hio ilimalizika kwa ushinde wa bao 1-0 kwa faida ya Royal kutokea Muramvya. Bao pekee la mchuano huo limepatikana kwenye kipindi cha kwanza bao lilofungwa na Eric Evra , Mchezaji wa ngome ya nyuma Eric evra,bao ambalo limeshangaza wengi kwani hakuna alietegemea kuwa litaingia wavuni. Ilikuwa ni mpira wakutengwa akawa ameupiga na moja kwa moja ukawa ume elekeya golini kipa akawa amepishana nao . match ya jana kati ya Atletico Olympic na Prince Louis ilimalizika kwa ushinde wa Atletico bao 2 kwa 0 ya Prince Louis . Wiki mbili zijazo tutashughudia pambano ya Vital'o fc na Enougou Rangers kwa upande wa Club bingwa barani africa . Lydia Ludic Burundi academic yao itakuwa jijini Kinshasa kupambana na Club ya D.C Motema Pembe . Duru kutoka kwenye shirikisho la dimba nchini ( FFB) limetangaza kuwa timu za daraja la kwanza ambazo hazishiriki kwenye mashindano hayo yakimataifa zitarejeya kucheza ifikapo tarehe 30/March match ya kombe la Raisi .

 Matokeo 
--------------
Jumaa-mosi : Prince Louis 0 - 2 Atletico Olympic
Jumaa-pili : Flamengo 0 - 1 Royal fc

Msimamo wa wiki ya 11 (Duru ya awali)
--------------------------------------------------
 1. Athletico Olympic 23 points
2. Vital'o fc 22 points
3. Flambeau de l'Est 22 points
4.Royal fc 19 points
5. Lydia Ludic Bdi Academic 18 points 

6. Muzinga 17 points
7. Academie Tchite 15 points
8. Inter stars 12 points
9. Prince Louis 12 points 

10. Messagers 12 points
11. Flamengo fc 7 points
12. Espoirs 5 points

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire