lundi 1 avril 2013

FABRICE BIRORI :" Video 8 zangu mpia zitakufikieni hivi karibuni..."

Msanii wa miondoko ya hip hop toka nchini Burundi BIRORI FABRICE amelonga na BB akawa ametuwekea wazi kuwa yuko kwenye harakati zakumalizia mlolongo wa picha zakuona (video) za nyimbo zake 8 na vile vile kuachia leo hii pini yake mpia itakayosimama na jina la "Abantu nkamwe" aliomshirikisha WILLY SIRABAHENDA mmoja kati ya wasanii waliokuwa wanaunda kundi la Etoile du Centre . Alitwambia :" Niko natumika na Golden Star pamoja nae KOOK KAY videos nane , hivi karibuni zitakuwa zimemalizika ,ni na imani kuwa Washabiki wangu watapa uhondo tosha kwani tumetumia ufundi wa hali ya juu ,tumejitaidi kadri na uwezo wetu kuonyesha hali halisi ya vituko , ushauri wa maneno tuliokuwa tunaimba kwenye nyimbo hizi 8 ambazo ni pamoja na 1.Reka nkwibarize 2.Ubwoko bwimamba 3.Abantu nkammwe 4.Africa 5.Ntibakiri isoko 6. Mama 7. Tamaa 8. itangazo ..." Ifahamike ya kwamba FABRICE BIRORI yumo katika kundi la Bold Boys pamoja nae Chris B NDINDI

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire