dimanche 31 mars 2013

Primusic : Tamasha yakusaidia waliopoteza mali zao soko ilipo unguwa ilifanyika leo ku EFI...


Leo tarehe 31/March/2013 ni siku waumini wa dini ya kikristo wanakumbuka kufufuka kwa JESUS ndipo BRARUDI kampuni ya vinywaji tofauti tofauti kupitia  kinywaji PRIMUS kwa ushirikiano na waimbaji wa mitind ya buja flava wameendesha bonge la Tamasha kwa niaba ya walio poteza bidhaa zao na vitu vyote baada yakutokomea kwa soko kuu ya Bujumbura ilipo . Kwa muujibu wa habari tulio ipata kwa walio anda tamasha hio walitwambia kuwa shaba kubwa nikuwakumbuka waliopoteza mali zao , na vile vile kuwaburudisha raia wa Burundi kwani Bujumbura iko kama imelala . Kwenye tamasha hio wanamuziki walionyesha ushirikiano tosha kwani asilimia 100 ya wasanii wote waliokuwa kwenye bango na ata wenye hawakuwa waliwasili ili kuonyesha ushirikiano wao . Peace & love , Baoden , Jay Fire ,Saidi Brazza , Mkomboz , Big Fizzo , Pidco & Crespinho , Emelance Emy , Ell's boy , Yoya ,Pop G , Sat B, Rally Joe ,  T max , Kiki Toure , Matabaro patient , Master Land , Kidum na wengine wengi walikuwepo... Kati yao wengi wali imba live music ila kuna baadhi ya wanao ondoka na mitindo ya Hip hop iliwawea ngumu kuimba live . Farious , Baoden , T Max , Jay fire   walitumia Cd , Sat b alichanga cd na live , wengine walitumia alaa (Instruments). Watu hawakuwa wengi tukilinganisha na fainali ya mwaka jana , tatizo hatukujuwa ilikuwa nini , tunawaza kuwa yaweza kuwa ni tatizo la kibaridi cha mvua mvua iliokuwa inatinga Bujumbura ao ki ingilio ambacho hakizoweleki sana kwa Washabiki wa Tamsha mbali mbali...
Kwa upande wakiufundi mambo yalikuwa mazuri tukilinganisha  na fainali iliofanyika tarehe 22/December/2012 ulikuwa wakuridhisha kama mnavyo jionea kwenye picha hizo apo , lakufurahisha zaidi ni kuona kuwa walifkiria hata kuileta gari lakuzima moto , gari lakuwaisha wagonjwa hospitalini ( Ambulance ) ni jambo lakuridhisha mno . Fahamu vile vile ya kuwa wasanii wote walio imba hakuna hata pesa tano walipewa bali nikujitolea kwao . Ni jambo nzuri walilofikiria kulifanya viongozi wa brarudi... fahamu ya kuwa nyimbo ya KIDUM na RALLY JOE inayojulikana kwa jina "IMPANURO" iliotengenezwa na R KAY nchini Kenya ipo tayari na kwa mara ya kwanza ili imbwa live siku ya leo,video ilitengenezwa na OGOPA Video na iko tayari kwenye mtambo wa kijamii Youtube...
Emelance Emy

N.B: Kutokana na ufundi kidogo kutoturaisishia kazi kuna baadhi ya picha zenye hatukuziweka kwenye habari hii...

Aucun commentaire:

Enregistrer un commentaire